Header Ads

Watu 8 wanusurika kifo baada ya kunywa maziwa yanayosemeka yalikuwa na sumu....

Watu 8 wa familia tatu tofauti akiwemo mama mjamzito wa kijiji cha Nkuhi wilayani Ikungi,wamenusurika kufa baada ya kunywa maziwa yanayo sadikiwa kuwa na sumu.
Wakijieleza kwa shida akiwemo aliyewauzia maziwa hayo huku wakiwa wamelazwa katika hospitali teule ya masister wa malikia wa ulimwengu iliyopo katika kijiji cha Puma ,wamesema baada ya kunywa maziwa hayo walianza kuumwa na tumbo huku wakiharisha na kutapika kwa mfululizo

Mganga mfawidhi wa hospitali teule ya masister wa malikia wa ulimwengu Daktari Corbinian Nyenyembe,wamekiri kuwamepokea wagonjwa hao walio sadikiwa kunywa maziwa yenye sumu, wa familia tatu akiwemo mama  mjamzito.

Bwana Jeremia Saudi ni baba wa watoto 3 walio kunywa maziwa na wamelazwa katika hospitali hiyo ,amesema wamebaini kuwa maziwa hayo yanaweza kuwa na sumu baada ya kaka yake kuyafanyia uchunguzi maziwa hayo.

No comments

Powered by Blogger.