Header Ads

Mmoja wa kikundi cha Panya Road auwawa Ukonga Mombasa

Kwa taarifa za muda huu ni kwamba vijana wa panya road Maeneo ya Ukonga Mombasa kwa diwani waliokuwa wamemvamia muendesha boda boda wakiwa na visu ameuawa mmoja wa panya road na mwili wake unaelezwa upo eneo hilo na bado jeshi la polisi halijafanikiwa kuuchukua.
Hali hii inaleta sinto-faham baada ya kamanda wa polisi Suleiman Kova kuwaondoa wasi wasi watanzania juu ya kuwepo kwa panya road nakusema ni uvumi tu,na kuwaasa wananchi kutokujichukulia sheria mkononi na pindi wanapo mkamata mhalifu wamfikishe kituo cha polisi.

No comments

Powered by Blogger.