Header Ads

MWENYEKITI WA CCM,RAIS JAKAYA KIKWETE AWASILI JIJINI MBEYA JIONI YA LEO TAYARI KWA KUONGOZA MAADHIMISHO YA MIAKA 37 YA CCM KESHO.

 Mwenyekiti wa  CCM,Rais Jakaya Kikwete akiwapungia Viongozi mbalimbali wa chama,Serikali,viongozi wa dini na watu mbalimbali (hawapo pichani) waliofika kumpokea mara baada kuwasili jioni ya leo kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe  tayari kwa kuongoza maadhimisho ya sherehe za miaka 37 ya chama hicho yatakayofanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu wa Sokoine mjini humo.

 Pichani Kati ni Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Kikwete akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa chama hicho,Ndugu Kinana (kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya na Mbunge wa jimbo la Mbozi Mashariki,Mh Godfrey Zambi mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Songwe jioni ya leo.

Pichani kati Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Kikwete pamoja na Viongozi wa ngazi za juu wa chama hicho,kulia ni Katibu Mkuu wa chama hicho,
Ndugu Kinana,Makamu Mwenyekiti Taifa,Mh.Phillip Mangulla na shoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya na Mbunge wa jimbo la Mbozi Mashariki,Mh Godfrey Zambi wakiwa kwenye kikao cha wanachana mbalimbali wa chama hicho (hawapo pichani) ndani ya ofisi ya makao makuu jijini Mbeya jioni ya leo mara baada ya kuwasili.

 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akilakiwa na waendesha boda boda kutoka sehemu mbali mbali,alipowasili kwenye uwanja wa Kimataifa wa Songwe,jijini Mbeya mapema leo wakati alipokwenda kumpokea Mwenyekiti wa chama cha CCM,Rais Jakaya Kikwete aliyewasili jioni ya leo kwa ajili ya kuhserehekea maadhimisho ya miaka 37 ya chama cha CCM yatakayofanyika katika uwanja wa Sokoini mkoani humo.
 Katibu wa Uchumi na Fedha Bi.Zakia Meghji akizungumza jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais asiye na Wizara maalum na Mbunge wa jimbo la Rungwe Mashariki,Mh.Prof.Mark Mwandosya walipokutana jioni ya leo kwenye uwanja wa Ndege wa songwe walipokuwa wakimsubiri Mwenyekiti wa chama cha CCM,Rais Jakaya Kikwete aliyewasili leo jioni tayari kwa kuongoza maadhimisho ya sherehe za miaka 37 ya chama hicho yatakayofanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu wa Sokoine mjini humo.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana pichani kushoto akizungumza jambo kwa msisitizo na Waziri wa uchukuzi Dr.Harrison Mwakyembe,ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Kyela walipokutana jioni ya leo kwenye uwanja wa Ndege wa  Kimataifa wa Songwe walipokuwa wakimsubiri Mwenyekiti wa chama cha CCM,Rais Jakaya Kikwete aliyewasili leo jioni tayari kwa kuongoza maadhimisho ya sherehe za miaka 37 ya chama hicho yatakayofanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu wa Sokoine mjini humo.

No comments

Powered by Blogger.