SIMBA YA JUU LEO DHIDI YA Oljoro JKT
Kikosi cha Simba
AMISI Tambwe
amedhihirisha nia yake ya kunyakua kiatu cha dhahabu baada ya jioni hii
kufunha 'hat trick' yake ya pili msimu huu wakati Simba ikipata ushindi
wa mabao 4-0 dhidi ya Oljoro JKT.
Mabao hayo yamemfanya mshambuliaji huyo
kutoka Burundi kufikisha jumla ya mabao 13 na kuwakimbia Elias Maguli wa
Ruvu Shooting na Kipre Tchetche wa Azam wenye mabao tisa kila mmoja
wanaomfukuzia katika magoli.
Simba ilitawala pambano hilo lililochezwa
kwenye uwanja wa Taifa kwani ilianza kuandika bao la kwanza dakika ya 12
tu kupitia Jonas Mkude kabla ya Tambwe kuanza vitu vyake kwa kufunga
mabao mawili yaliyofanya Mnyama aende mapumziko wakiongoza 3-0.
Tambwe laifunga bao la kwanza kwake na la
pili kwa Simba dakika ya 24 kabla ya kuongeza jingine dakika ya 29 na
kuja kupiga 'hat trick' yake ya pili baada ya ile ya kwanza alipoifumua
Mgambo kwa magoli yake manne mwaka jana.
Bao hilo la tatu kwake na la nne kwa Simba
lilifungwa katika dakika ya 52 akiunganisha krosi ya winga Haruna
Chanongo kablka ya kutolewa baadaye na nafasi yake kuchukuliwa na
Abdulhalim Humud 'Gaucho'.
Kwa ushindi huo Simba imefikisha pointi 30
na kuendelea kusalia nafasi ya nne nyuma ya Mbeya City ambayo kesho
itaikabili Yanga wenye pointi 32 katika pambano jingine linalosubiriwa
kwa hamu.
Oljoro inayonolewa na kocha wa zamani wa
Coastal Union, Hemed Morocco ilikosa mabao mengi ya wazi katika pambano
hilo na hasa kwa mashambuliaji wake Shija Mkina aliyewahi kung'ara na
Simba.
Tofauti na mechi yao ya Mgambo, leo Amisi
Tambwe alipewa mpira wake na mwamuzi Nathan Lyimo mara baada ya mchezo
huo kuisha kwa kupiga hat trick ambayo inakuwa ya tatu, nyingine
ilipigwa na Abdalla Juma wa Mtibwa Sugar..
No comments