ANGALIA VIDEO YA MWANAUME ANAYEWEZA KUKAANGA KUKU KWENYE MAFUTA KWA MIKONO YAKE BILA KUUNGUA
Mwanaume huyo (52) mkazi wa jiji la Chiang Mai ambaye ni mpishi
huko Thailand, ana uwezo wa ajabu wa kuzamisha mikono yake katika mafuta
yenye moto wa digrii 480 bila kuungua na amedai kuwa huwa hasikii
maumivu ya aina yoyote wala ngozi ya mikono yake haidhuriki na mafuta ya
moto mkali.
Mr Trichan anashikilia rekodi ya dunia kwa kukaanga vipande 20 vya kuku katika mafuta ya moto wa 480c ndani ya dakika 1.
Kutokana na maajabu hayo ya mikono yake mwanaume huyo amepata
umaarufu wa kimatifa uliompa faida zaidi katika biashara yake kwani watu
mbalimbali kutoka pande tofauti za dunia wamekuwa wakitembelea ofisi
yake ya chakula “Fried Chicken Iron Hands Man” ili kushuhudia jinsi Kann
anavyoweza kutumia mikono yake kuchota kuku kutoka kwenye mafuta ya
moto.
Mwanaume huyo na mke wake wamekuwa wakisafiri duniani kuonesha
maajabu hayo ambayo hajui ni jinsi gani ameweza kufanya anachokifanya na
mikono yake, lakini anafuraha sababu inamuongezea wateja zaidi katika
biashara yake kila siku.
Mr Trichan aligundua kipaji chake hicho cha kipekee miaka nane
iliyopita baada ya kumwagikiwa na mafuta ya moto kwa bahati mbaya lakini
hakudhurika.
Onyo: Usijaribu hii nyumbani.
Angalia video yake kwa kubofya play hapa chini...
No comments