Header Ads

ARSENAL YALIPA KISASI KWA LIVERPOOL, YAITOA KOMBE LA FA JIONI HII 2-1

BAO la Alex Oxlade-Chamberlain na pasi ya bao vimetoa mchango mzuri jioni hii kwa Arsenal kutinga Raundi ya sita ya Kombe la FA baada ya kuifunga Liverpool mabao 2-1 Uwanja wa Emirates.
Kiungo huyo kinda wa England alifunga bao la kwanza dakika ya 16 akimalizia pasi ya Lukas Podolski, aliyefunga bao la pili dakika ya 47.
Refa Howard Webb aliwapa penalti Liverpool baada ya Podolski kumchezea faulo Luis Suarez, na Steven Gerrard akaenda kufunga dakika ya 59.
Pamoja na hayo, Webb alimezea penalti nyingine ya Liverpool baada ya Oxlade-Chamberlain kumuangusha Suarez kwenye eneo la hatari.
Liverpool ilitawala mchezo na kutengeneza nafasi nyingi za kusawazisha, lakini mwisho wa mchezo, Arsenal walifanikiwa kulipa kisasi cha kufungwa mabao 5-1 Uwanja wa Anfield katika Ligi Kuu.


Kitu hicho: Alex Oxlade-Chamberlain akifunga bao la kwanza

Anashangilia


Luis Suarez akiwa haamini macho yake baada ya refa Howard Webb kuwanyima Liverpool penalti ya pili.

kikosi cha Arsenal: Fabianski, Jenkinson, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Flamini, Arteta, Oxlade-Chamberlain (Gibbs 76), Ozil, Podolski (Cazorla 69), Sanogo (Giroud).
Subs not used: Sagna, Wilshere, Viviano, Gnabry

kikosi cha Liverpool:
Jones, Flanagan, Agger, Skrtel, Cissokho (Henderson 62), Coutinho, Gerrard, Allen, Sterling, Suarez, Sturridge.
Subs not used: Toure, Aspas, Moses, Mignolet, Kelly, Teixeira. 

No comments

Powered by Blogger.