DIRISHA LA USAJILI LAFUNGWA RASMI: Fullham,Sunderland,Arsenal na Chelsea wamekamilisha Usajili
Kujiamini: Kurt Zouma amejiunga na Chelsea lakini atabakia St Etienne kumalizia msimu
MOURINHO ASAINI BEKI LA KATI CHELSEA KINDA LA MIAKA 19 KUTOKA UFARANSA
KOCHA Jose Mourinho amekamilisha usajili wa Kurt Zouma kutoka klabu ya St-Etienne.
Chelsea
imekubali kulipa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 12.5 kwa ajili ya beki
huyo wa kati kinda wa umri wa miaka 19, ambaye atabakia Ufaransa
kumalizia msimu.
FULHAM YAMSAINI LEWIS KUTOKA SPURS KWA MKOPO
KLABU ya Fulham imethibitisha kumsajili kwa mkopo Lewis Holtby kutoka Tottenham.
Kiungo huyo amekuwa akisotea namba kikosi cha kwanza Spurs tangu awasili kutoka Schalke Januari mwaka jana.
Atabakia
Craven Cottage hadi mwishoni mwa msimu, na anakuwa mchezaji wa tatu
kusajiliwa na Rene Meulensteen katika dirisha hili lausajili.
Fullham pia imemsajili Mitroglouili kuziba pengo la dimitar Berbatov aliye timkia Monaco
KIUNGO wa
Arsenal, Emmanuel Frimpong amesaini klabu ya Daraja la Kwanza Barnsley
from Arsenal kwa ada ya uhamisho ambayo haikutajwa.
Baada ya
kusaini timu hiyo, kinda huyo akatweet: "How am I gonna draw girls now"
akimaanisha atakuwa na wakati mgumu mno kuwavutia mademu - ingawa baada
ya muda mfupi tu akafuta.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 amesaini kupiga kazi Oakwell hadi Juni 2014.
Nitapataje mademu sasa: Emmanuel Frimpong akiwa na jezi ya Barnsley baada ya kusaini akitokea Arsenal
SUNDERLAND YASAINI KIUNGO MPYA
KIUNGO
Liam Bridcutt amekamilisha usajili wa Pauni Milioni 2.5 kutua Sunderland
akitokea Brighton, akiwa mchezaji wa tano kusajiliwa na Gus Poyet
dirisha hili la usajili.
Kiungo
huyo mwenye umri wa miaka 24, alisafiri kwenda Wearside Alhamisi
kujadili usajili wake na Black Cats ambao aliukamilisha leo asubuhi.
No comments