ANGALIA PICHA YA MWANAUME ALIYEJIBADILISHA JINSIA AKITAKA VYETI VYAKE VIBADILISHWE MAJINA
Afisa Mkuu Mtendaji wa Baraza la Kitaifa la Mitihani (KNEC) Paul Wasanga.
BAADA YA KUJIBADILISHA |
BAADA YA KUJIBADILISHA |
MWANAUME
aliyegeuza jinsia yake, amelishtaki baraza la mitihani nchini, Kenya
National Examination Council (KNEC), akitaka lishurutishwe kubadilisha
vyeti vyake kuonyesha kwamba ni mwanamke.
Bi
Audrey Mbugua ambaye awali alifahamika kwa jina la Andrew Ithibu kabla
ya kubadilisha jinsia yake, anataka cheti chake cha mtihani wa kidato
cha nne (KCSE) kionyeshe kwamba ni mwanamke.
Aliambia
mahakama kwamba aligunduliwa kuwa na dosari ya jinsia 2001, na amekuwa
akikabiliana na shida nyingi kwa sababu anatambuliwa kama mwanaume
katika vyeti vyake.
“Nimejaribu
kuomba KNEC mara nyingi ibadilishe jina langu katika cheti changu vya
mtihani wa KCSE ili kionyeshe jinsia yangu halisi bila kufaulu,” Bi
Audrey aliambia mahakama.
Alisema
hatua ya KNEC kukataa kufanya mabadiliko hayo, imemsababishia mateso
mengi kwa kubaguliwa na kunyimwa kazi. Mahakama ilimruhusu kuwasilisha
ombi la kutaka baraza hilo liagizwe kutekeleza majukumu yake kwa
kurekebisha jina lake liwe na mwanamke.
Siku 14
Anataka
pia baraza hilo iagizwe kubadilisha alama inayoonyesha jinsia yake
inayoonyesha ni mwanaume katika cheti hicho na badala yake ionyeshe kuwa
ni mwanamke.
Mahakama ilipatia KNEC na Mkuu wa sheria muda wa siku 14 kujibu ombi la Bi Audrey.
Kesi itatajwa Mei 28 ili mahakama itoe maagizo zaidi.
No comments