Header Ads

Wachimba Mgodi 5 wafariki mkoani Geita

Wachimbaji dhahabu watano wamefariki baada ya kufukiwa na kifusi katika machimbo ya Mgusu mkoani Geita.

Mwandishi wetu anaarifu kuwa ,tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Jumapili katika machimbo yanayomilikiwa na kampuni ya Geita Gold Mine ambayo ni moja ya makampuni makubwa ya uchambaji wa dhahabu barani Afrika.

Makamu wa rais wa kampuni hiyo Simon Shayo amemwambia mwandishi wetu kwamba miili hiyo iliokolewa jana kwa ushirikiano na wachimbaji wengine wa eneo hilo.

Shayo alisema eneo ambalo tukio hilo lilitokea si eneo salama na kwamba lilipigwa marufuku kwa shughuli za uchimbaji.

Hata hivyo baadhi ya wachimbaji wamekuwa wakiendelea kuingia na kufanya shughuli za uchimbaji kinyemela na kupuuza ilani ya kutoingia katika maeneo hayo.

No comments

Powered by Blogger.