Header Ads

Waasi waua watu 38 Mashariki mwa Congo

Watu 38 waliuawa hapo jana katika makabiliano kati ya majeshi ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na wanamgambo wa kiislamu kutoka Uganda.

Umoja wa mataifa umesema kuwa wanamgambo wanaoshukiwa kuwa wa kundi la ADF-NALU walishambulia kambi ya kijeshi ya umoja wa mataifa na ile ya serikali ya DRC jana usiku na kuua askari mmoja wa kulinda amani pamoja na raia 15.

Jenerali Jean Baillaud, ameiambia BBC kuwa hili ndilo shambulizi baya zaidi dhidi yao katika kipindi kirefu.

Mtu mmoja aliyeshuhudia mapigano hayo amesema wanamgambo walishambulia wagonjwa na wafanyikazi katika hospitali moja Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.

Wengine walikuwa wamejihami kwa bunduki huku wengine wakiwa na mapanga.

Asilimia kubwa ya wenyeji wapatao elfu 20,000 wa mji huo wa Eringeti wametorokea usalama wao kufuatia shambulizi hilo lililoanza mwendo wa saa kumi jioni kwa uvamizi wa makumi ya wanamgambo.

Walipora maduka na nyumba zilizokuwa na chakula.

Waasi wameshtumiwa kwa kusababisha vifo vya watu wapatao mia tano katika muda wa miaka miwili.

Credit: BBC

No comments

Powered by Blogger.