Header Ads

Mkutano, Kinana akiwa Kilimanjaro kumnadi Dr. Magufuli

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana ameongoza timu ya chama hicho kumsafishia njia Mgombea Urais wao, Dk John Magufuli mkoani Kilimanjaro, huku akiwaambia wananchi wa mkoa huo kuwa mgombea huyo ndiye kiongozi anayestahili kuongoza Tanzania.

Akizindua kampeni za CCM mjini Moshi, Kinana aliongozana na mgombea ubunge wa Jimbo la Simanjiro mkoani Manyara, Christopher ole Sendeka na yule wa Mtera mkoani Dodoma, Livingstone Lusinde maarufu kama Kibajaj.

Kinana alimuelezea Magufuli kuwa ni kiongozi anayestahili kuongoza Tanzania kutokana na historia yake ya uadilifu na uchapakazi katika maisha yake yote ya utendaji serikalini. 


Alisema katika utendaji wake akiwa Waziri kwa miaka 20, amefanya kazi kubwa kwa uadilifu na kujituma.

Akimuelezea zaidi Magufuli, Kinana alisema mgombea huyo ameahidi Baraza dogo la Mawaziri, hajatumia fedha kupata nafasi ya kugombea urais wala hana makundi.

“Hana makundi...wapo waliochangisha fedha wamekusanya watu baadaye wanakuja kuwa mzigo.

"Yeye Hana makundi wala hana mzigo. Hajaenda wilayani ama mikoani bali alienda matawini,” alieleza Kinana ambaye pia alimuombea kura mgombea ubunge Jimbo la Moshi Mjini, Davis Mosha.

Kwa upande wake, Ole Sendeka alisema ni lazima Watanzania wawapime wagombea kwa kujua ukweli, si kwa kudanganyana na kuepuka dhambi ya ubaguzi wa aina yoyote.

No comments

Powered by Blogger.