Header Ads

Maneno ya Diamond Platnumz baada ya kutajwa kuwania tuzo ya MTV Europe Music Awards 2015

Naseeb Abdul aka Diamond Platnumz amepata nafasi ya kuipeperusha bendera ya Tanzania katika tuzo za MTV Europe Music Awards 2015 zitakazotolewa mwezi October 25, 2015 jijini Milani Italy.
Msanii huyo ambaye ametajwa kuwania tuzo ya MTV Europe Music Awards katika kipengele cha Best African Act, akiongea na ripota wa millardayo.com alisema..‘Kiukweli namshukuru sana mwenyezi Mungu kwasababu najua mimi naamini sio mimi tu watanzania wengi ndoto zenu ni kuomba muziki wetu uweze kutambulika kimataifa sio tu kutambulika bali kupewa heshima kwa taifa letu la Tanzania‘ – Diamond Platnumz

Kwasasa mambo yanaenda vizuri kabisa kwa hiyo kuteuliwa katika tuzo za MTV Europe kwangu ndio mara yangu ya kwanza pia hata kwa Tanzania, namshukuru Mwenyezi Mungu nauzuri tuzo hizo haziangalii chochote kwani zinaangalia kura za watu so naamini muda ukifika basi mashabiki tupige sana kura ili tuweze kufanikiwe kuuleta ushindi nyumbani, nakumbuka mwaka jana walishinda Sauti Sol‘ – Diamond Platnumz

No comments

Powered by Blogger.