Header Ads

Lowassa aweka historia katika viwanja vya barafu jana mkoani Dodoma

Lowasa katika viwanja vya BARAFU dodoma leo ameweka Historia katika mkutano huo kwa umati mkubwa wa watu uliojitokeza kumlaki na kumsikiliza.

Mgombea urais wa UKAWA Mh Edward Lowassa amesema akichaguliwa kuwa rais wa awamu ya tano ataunda serikali itakayokuwana viongozi wenye uwezo wa kuchukua hatua na kutatua matatizo ya wananchi na atahakikisha utaratibu wa wananchi kulalamika na viongozi pia kulalamika kama ilivyo sasa unabaki kuwa historia.

Mh Lowassa ambaye amefanya mikutano minne katika majimbo ya Mtera, Bahi Chilonwa na Dodoma mjini pia amewaomba watanzania kumpa nafasi ya kukamilisha ndoto yake ya kuleta usawa wa huduma zakijamii ikiwemo elimu aliyoanza kuonyesha mfano kupitia shule za kata alipokuwa waziri mkuu.
Awali waziri mkuu mstaafu wa awamu ya tatu Mh Fredrick Sumaye na mwanasheria wa Chadema Mh Tundu Lisu wamesema kukithiri kwa malalamiko ya wananchi kukosa huduma huku wanaotakiwa kuchukua hatua wakiendelea kutoa ahadi inatosha kuonyesha kuwa uwezo wao wa kupata ufumbuzi umefika mwisho na ndio maana UKAWA inaomba nafasi ya kuondoa tatizo hilo.

Wananchi na viongozi wa jimbo la Mtera wamesema ubinafisi wa viongozi wa CCM, na ahadi zisizotekelezeka umesababisha wapoteze matumaini ya kuondokana na umaskini hasa kwa vijana suala ambalo aliyekuwa naibu waziri wa kazi na ajira Dr Makongoro Mahanga ambaye sasa amehamia UKAWA analitolea ufafanuzi.


Akihitimisha mikutano yake ya kampeni katika mkoa wa Dodoma uliofanyika Dodoma mjini Mh Lowaasa ambaye sasa anaelekea mkoa wa singida ameendelea kunadi sera za UKAWA na kutoa ufafanuzi wa namna ya kuzitekeleza kwa wakati na kwakasi inayostahili.


No comments

Powered by Blogger.