Tibaijuka.. Nitagombea Ubunge Mwakani licha ya Sakata la Escrow..
Siku chache baada ya Rais Kikwete kumfuta kazi Tibaijuka kama waziri wa ardhi,nyumba na makazi ,mbunge huyo amewaambia wapiga kura wake kwamba hawakumchagua kama waziri bali kama mwakilishi wao.
Tibaijuka alifukuzwa kazi na Rais Kikwete kufuatia kashfa ya akaunti ya tageta escrow ambapo alipokea sh.billioni 1.6.

''Mungu anayetoa ndiye aliyechukua jina la mungu libarikiwe", alisema tibaijuka akimaanisha kuwa yule aliyempa kiti hicho cha uwaziri ndiye aliyekichukua.
Katika kile alichoelezea kama harakati za kukitetea kiti chake katika uchaguzi wa 2015,Tibaijuka aliwaonya wapinzani wake wa kisiasa kwamba yeye ndiyo chagua bora la wapiga kura.
Tibaijuka aliwashukuru wapiga kura wake kwa kumchagua kuwa mbunge,wadhfa aliodai kumfungulia milango ya kupewa uwaziri.
''Lazima muelewe kwamba ninyi mlinipigia kura mimi ili niwahudumie bungeni na sio kama waziri,kwa hivyo yaliotokea si ndwele tugange yajayo kwa kuwa tayari kashfa ya escrow imezikwa'',aliwaambia wakaazi wa Muleba.

No comments