Header Ads

Mahaba!!! Kim Kardashian avunja ndoa ya Mtu ...Kisa hiki hapa

Mwanamke mmoja ambaye jinalake ni Rahma, kutoka Cairo, Misri, amedai talaka kwa mumewe kwa kuwa amekuwa si mwaminifu, amekuwa akimsaliti mara kwa mara kutokana na kile ambacho mwanamke huyo amekisema eti mumewe anataka mke wake afanane na Kim Kadarshian au muigizaji Haifa Wehbe.
Mara kadhaa mume wa mwanamke huyo amekuwa akimtaka avae na kutengeneza nywele zake ili afananena mmoja ya mastaa hao, alikataa, amesema anatazama mambo mengine ya msingi kuyafanya ikiwemo kumlea mtoto wake wa mwaka mmoja, hivyo asingeweza na hili la kujitengeneza ili afanane na mastaa hao ambao yeye aliwaita midoli wa kwenye TV! 
Kwa kuwa dini ya mwanamke huyo inaongozwa na Sheria ya Shariah ambayo inaruhusu mwanamke kuachika na mahari iliyotolewa kurudishwa, mwanamke alifanya maombi ya kudai talaka ili aendelee na maisha yake mengine.

No comments

Powered by Blogger.