Header Ads

Chelsea waitwangwa Crystal Palace 2-1

Chelsea imeendelea kujikita kileleni mwa Ligi Kuu ya England baada kupata ushindi mwembamba wa 2-1 kutoka kwa Crystal Palace huku beki wake wa kushoto Azpilicueta akilambwa kadi nyekundu dakika ya 40.
Vijana wa Jose Mourinho sasa wanakuwa wamejikusanyia jumla ya pointi 22 katika michezo minane walioyocheza huku City ikifuatia kwa pointi 17.

Mashujaa wa Chelsea katika mchezo huu walikuwa ni Oscar aliyefunga dakika ya pili pamoja na Fabregas aliyepachika goli la pili katika dakika ya 51. Bao la Crystal Palace lilifungwa na Campbell dakika ya 90. 








Crystal Palace: Speroni, Kelly, Hangeland, Delaney, Ward, McArthur, Jedinak, Ledley, Puncheon, Campbell, Bolasie.

Chelsea: Courtois, Ivanovic, Terry, Cahill, Azpilicueta, Matic, Fabregas, Willian, Oscar, Hazard, Remy.

No comments

Powered by Blogger.