Angalia picha za mechi ya Simba na Yanga taifa leo
Askari wa Farasi kutoka Kikosi cha FFU wakiwa katika doria kabla ya kuanza mchezo. (Picha na Francis Dande)
Beki wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ (kulia), akipambana na
mshambuliji wa Simba, Elius Maguri (katikati) huku Kelvin Yondani wa Yanga
akiwa tayari kutoa msaada wakati wa mchezo namba 27 wa Ligi Kuu ya Soka
Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Timu
hizo zilitoka sare ya bila kufungana.
Kipa wa Yanga Deogratias Munishi akiokoa mpira.
Mshambuliaji wa Simba, Elius Maguri akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Yanga, Oscar Joshua (kulia).
Kocha wa Simba, Patrick Phir akiingia uwanjani.
Shabiki wa Simba.
Waamuzi wa mchezo huo.
Mashabiki wa Simba wakimpa fedha kipa wa Simba, Manyika Peter baada ya kuokoa hatari nyingi langoni mwake.
No comments