Header Ads

Wanusurika kifo katika kituo cha Ouality plaza-Dar

Abiria waliokuwa katika kituo cha mabasi eneo la Quality Plaza jijini Dar wakisubiri usafiri wamenusurika kifo baada ya gari aina ya Toyota Raum lenye namba za usajili T483 CMU, kuhama njia katika barabara ya Nyerere na kuparamia kituo hicho.
Gari aina ya Toyota Raum lenye namba za usajili T483 CMU likiwa eneo la kituo cha mabasi.
Dereva wa gari lililopata ajali ambaye jina lake halikufahamika mara moja akiongea na simu.

Dereva wa gari hilo mwenye asili ya Kihindi ambaye jina lake halikufahamika mara moja alishindwa kulimudu ndipo lilipovuka ukingo unaotenganisha barabara hiyo na kuhamia upande wa pili kisha kuparamia kituo cha abiria. Katika ajali hiyo hakuna mtu aliyejeruhiwa.
Tairi likiwa limepasuka baada ya ajali hiyo.
Mashuhuda wakiwa eneo la tukio.

No comments

Powered by Blogger.