Header Ads

JK amemteua Prof. Mwandosya kuwa chansela wa chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST)

www.paparaziwetu.blogspot.com
Raisi Jakaya Kikwete amemteua Waziri wa nchi,Ofisi ya Raisi, Prof Mark Mwandosya,kuwa Chansela wa chuo kikuu cha sayansi na Teknologia Mbeya(MUST).

Katibu mkuu wa wizara ya mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Dk Patrick Makungu, alisema MUST imeboreshwa na kuwa na ngazi ya chuo kikuu kuanzia marchi 29, 2012 ambapo kabla ilikuwa ikijulikana kama Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Mbeya (MIST).

"Ni heshima kubwa kuteuliwa na Raisi kama Chansela wa chuo kimpya," alisema Prof Mwandosya jana kwa njia ya simu akiwa India ambapo alikwenda wiki iliyopia kwa utaratibu wake wa kuangalia afya yake.
www.paparaziwetu.blogspot.com
Prof. Mwandosya aliongeza kwa kusema" Mimi nitalipa heshima hii kwa kufanya kazi kwa karibu na mwenyekiti wa Baraza la chuo, Prof Penina Mlama, Makamu Prof Msambichaka,seneti,wahadhiri na jamii yote ya chuo kikuu kwa ajili ya kufikia malengo yaliyokusudiwa"
www.paparaziwetu.blogspot.com
Vile vile alisema " Ni heshima kubwa kwake kujiunga na klabu ya machansela wa vyuo vikuu akiwemo marehemu Fulgence Kazaura ambaye alikuwa chanesela wa chuo kikuu cha Dar es Salaam na wastaafu Rais Benjamin Mkapa, chansela kwa Chuo Kikuu cha Dodoma. Wengine ni Al Noor Kassum ya Chuo Kikuu cha Sokoine katika mkoa wa Morogoro, Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Muhimbili Allied, Makamu wa Rais Dk Mohamed Ghalib Bilal ya Nelson Mandela Taasisi ya Teknolojia na Waziri Mkuu mstaafu Cleopa Msuya wa Chuo Kikuu cha Ardhi. 
www.paparaziwetu.blogspot.com
Prof Mwandosya alishashika nyadhifa mbalimbali za uwaziri ikiwa ni pamoja na maji,mazingira, na mawasiliano na usafiri.

1 comment:

  1. Anonymous9:13 pm GMT+3

    Karibu sana professor,hapa huitwa home of Engineers

    ReplyDelete

Powered by Blogger.