Header Ads

Mwizi aliyechomwa moto baada ya kuiba pikipiki ..........Soma zaidi

Mtu mmoja anaesadikiwa kuwa ni jambazi ambaye hakufahamika jina anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 25 ameuwawa kwa kupigwa mawe kisha kuchomwa moto na mwingine kunusurika kuuwawa.

Tukio hilo limetokea alfajiri ya leo katika kijiji cha Shibula kata ya Bugongwa wilayani Ilemela Mkoani Mwanza kufuatia tukio la wizi lilotokea usiku wa kuamkia leo katika mtaa Nyamwilolelwa ambapo pikipiki moja na paneli ya solar ziliibiwa.

Katibu wa Sungusungu katika kijiji cha Shibula John Mashalia amesema kuwa kufuatia tukio hilo waliamua kuweka ulinzi shirikishi kuzunguka vijiji vyote na ndipo walipokutana na kijana huyo aliyeuwawa akiwa na kijana mwingine aliyefahamika kwa jina la Edward Aloyce ambao walidai wanatafuta pikipiki iliyopotea.

Mashalia ameongeza kuwa kata ya Bugongwa imekuwa na matukio ya ujambazi mara kwa mara ikiwa ni pamoja na vitendo vya ubakaji kwa watoto na wanawake.

Kwa upande wake mkaguzi msaidizi wa jeshi la polisi Joyce Kotecha amewataka wananchi wa kata hiyo kuacha kujichulia sheria mkononi na kwamba wawasiliane na uongozi wa kata yanapotokea matatizo ya namna hiyo.

Kijana aliyeuawa kwa kuchomwa moto.
Vijana wa sungusungu wakiwa katika mlango wa duka ambapo kijana mwingine aliyenusurika alifungiwa kungoja polisi.
Hii ni bodaboda ambayo walienda nayo eneo la tukio vijana hao. 
Polisi wakiwasili eneo la tukio.
Polisi wakipanga jinsi ya kumtoa mtuhumiwa huyo.
Mwili wa kijana huyo ukiwa chini baada ya moto kuzima.
Polisi wakipakia pikipiki iliyokutwa eneo la tukio.
 Polisi wakikagua makoti ambayo kijana aliyenusurika aliyavaa.
Wananchi waliojitokeza kushuhudia tukio hilo. 
Msaidizi wa polisi Inspector Joyce Kotecha akiwasihi wananchi watulie ili sheria ichukue mkondo wake.
Askari akiwa standby na bomu la machozi wakati wa kumtoa kijana aliyefungiwa dukani.
Kijana aliyenusurika aitwaye Mangi akitolewa ndani ya duka kwa ulinzi mkali na kupakiwa kwenye gari.

Kijana akiwa ndanin ya gari pembani ni maiti ya mwenzake.

No comments

Powered by Blogger.