Header Ads

Halima Kimwana mbabe wa Wema Sepetu aeleza haya kushusu Diamond na skendo......

Imeelezwa kuwa Diamond hapindui kwa halima kimwana kutokana na ukaribu wao wa mda mrefu, Wakati mpenzi wake Wema sepetu akiwa hapatani na kimwana kama paka na panya, hiyo haijasababisha Diamond kuwa mbali na kimwana, kwani ameshawahi kukiri kuwa hakuna atakayeweza kuwatenganisha na best wake huyo wa long time.

Kama ilivyo kwa kimwana, Diamond hawezi kupindua kwa wema sepetu, wakati kimwana yupo very close na familia ya Dangote, kitendo ambacho kinamuumiza zaidi madame kwani familia ya diamond imekuwa ikimchukia madame na kumkubali zaidi penny na halima, kitendo kinachomfanya penny awe karibu na kimwana kwni anajua fika diamond hapindui kwa kimwana.
Aliyejipachika kuwa dada wa hiyari wa Mbongo-Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye ni zao la Shindano la Kimwana Manywele, Halima Haruna ‘Kimwana’ amefungukia ishu ya mastaa kibao kujitongozesha wenyewe kwa jamaa huyo

Halima Kimwana alielezea sakata hilo wikiendi iliyopita baada ya kuulizwa undani wa skendo inayomkabili ya kumkuwadia au kumtongozea Diamond kwa mastaa na kuwabadilisha kama nguo.
Kwa mujibu wa Halima Kimwana, huwa Diamond hajisumbui kumtongoza mwanamke zaidi ya hao mastaa kujitongozesha wenyewe kwake.

Halima Kimwana alidai kwamba yeye kama dada wa mwanamuziki huyo (hakutaka kufafanua dada kivipi), amefikia hatua ya kusumbuliwa na wasichana wa kila aina hasa mastaa wakimuomba awatongozee kwa Diamond tena kwa ahadi kemkemu.
“Kwani unafikiri Diamond anajihangaisha kuwatongoza hao mastaa? Wao ndiyo kila kukicha wanamsumbua na kutuhangaisha sisi wakitaka tuwatongozee kwa kaka yetu.

Tena wengine wanatoa ahadi nyingi tu kama tukiwafanikishia,” alisema Halima Kimwana na kuongeza kuwa katika listi hiyo ya mastaa wanaojitongozesha kwa Diamond, wapo mastaa wakubwa ambao anawahifadhi ili asiwavunjie heshima.

No comments

Powered by Blogger.