UKATILI; MKE WA MTU AZAA NJE YA NDOA NA KUTUPA KICHANGA CHOONI IWAMBI MBEYA
Rukia Fungameza[20]mkazi wa mtaa wa Ilembo Kata ya Iwambi Anaetuhumiwa kutupa mtoto chooni |
Hii ndilo shimo la choo alimotumbukizwa mtoto huyo |
Wakina mama wakilia kwa uchungu |
Mwenyekiti wa mtaa huo Juma Mbuza mwenye Flana ya bluu akiwa na barozi kushoto na mashuhuda wengine wakimsikiliza mwenyekiti huyo |
Mwanamke
mmoja aliyefahamika kwa jina la Rukia Fungameza[20]mkazi wa mtaa wa
Ilembo Kata ya Iwambi anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya kwa
tuhuma za kutupa chooni kichanga jinsi ya kiume na kusababisha kifo
chake.
Mwenyekiti
wa mtaa huo Juma Mbuza amesema walimtilia shaka mtuhumiwa Februari 18
mwaka huu katika kilabu cha pombe za kienyeji baada ya kutoonekana na
ujauzito,ndipo walipomuulza kulikoni naye kudai kuwa amejifungua lakini
mtoto yupo nyumbani.
Kauli
hiyo haikumridhisha Mwenyekiti huyo ndipo alipoamua kumtafuta balozi
wake aitwae Daud Dule na kumuuliza mtoto yupo wapi ndipo alipoanza kuwa
na wasiwasi hali iliyowalazimu kumkamata kutoa taarifa kituo cha Polisi
Iyunga ambapo kabla ya kufika Kituoni majira ya saa kumi na moja jioni
mtuhumiwa alikiri kujifungua na kutupa kichanga chooni Februari 18 mwaka
huu.
Baada
ya taarifa hiyo mtuhumiwa alikamatwa na kupelekwa kituo kikuu cha kati
Febuari 19 ambapo Polisi hawakuweza kufika eneo la tukio licha ya
Mwenyekiti wa mtaa kufuatilia mara kwa mara kwa mkuu wa kituo cha Polisi
Iyunga ambapo alijibiwa kuwa watafika.
Hata
hivyo baada ya Polisi kutofika eneo la tukio kwa siku mbili tangu
kukamatwa mtuhumiwa Mwenyekiti wa mtaa alitoa taarifa katika kikao cha
kata Februari 21 kufuatia tukio lililotukia mtaani kwake na Polisi
kushindwa kufika kwenye tukio siku tatu baada ya tukio hali ambayo
ilikuwa kero mtaani kwake.
Polisi
walifika eneo la tukio Februari 22 majira ya saa tano na nsu asubuhi
wakiambatana na Kikosi cha Zimamoto Jiji la Mbeya ndipo walipoanza anza
kuibua mwili wa mtoto ambapo ulikutwa umeharibika vibaya kutokana na
kukaa kwa muda wa siku nne bila kuibuliwa umbali wa kilometa saba tu
kutoka Jijini.
Baada
ya mahojiano mtuhumiwa alidai sababu za kutupa kichanga hicho cha kiume
ni kutokana na kuogopa aibu kwa mumewe aliyepo Songea mkoani Ruvuma
kikazi ambapo mimba hiyo aliipata nje ya ndoa.
Uchunguzi
umebaini kuwa mwanamke huyo aliagizwa na mumewe kurejea Songea mwishoni
mwa mwaka jana lakini alikataa akidai kuwa angeenda mwaka huu baada ya
kumsaidia kaka yake shughuli za palizi.
Kabla
ya kichanga kilichotupwa chooni mtuhumiwa ana mtoto mwingine jinsi ya
kike anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka miwili na nusu.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Mtaa amelilalamikia Jeshi la Polisi kwa
kutoenda eneo la tukio mapema hali ambayo inasababisha wananchi
kujichukulia sheria mkononi hali ambayo inweza kuepukika.
Baadhi
ya mashuhuda akiwemo mama Emilly Amnoni na Paulo Mbawala wamelaani
vikali kitendo kilichofanywa na mwanamke huyo kwani wamedai ni cha
kinyama na ni cha kwanza mtaani kwao hivyo wanaomba sheria iweze
kuchukua mkondo wake ili kukomesha kabisa vitendo vya kikatili Mkoani
Mbeya.
|
No comments