Header Ads

TFF, WAFUTA GEMU YA YANGA NA PRISONS JUMATANO KUWAPA FURSA YA KUJIANDAA VYEMA DHIDI YA WAARABU

MECHI namba 118 ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga na Tanzania Prisons iliyokuwa ichezwe Februari 26 mwaka huu imehairishwa mpaka tarehe nyingine ilikuwapa nafasi ya kujiandaa vyema dhidi ya Al Ahly katika mechi ya marudiano huko Misri.

Uamuzi wa kuiondoa mechi hiyo iliyokuwa ichezwe Jumatano kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam umefanywa ili kuipa fursa zaidi Yanga kujiandaa kwa mechi yake ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi Al Ahly ya Misri itakayofanyika Jumamosi (Machi 1 mwaka huu). Al Ahly na Yanga zitarudiana wiki moja baadaye kati ya Machi 7, 8 au 9 mwaka huu jijini Cairo, Misri.

No comments

Powered by Blogger.