Header Ads

RATIBA YA UEFA EURO 2016 YAANIKWA


UEFA imetangaza Ratiba yote ya Mechi za Makundi ya EURO 2016 ili kusaka Timu 24 zitakazocheza Fainali huko Nchini France Mwaka 2016.

Mechi za Makundi zitaanza Septemba 7, 2014. Pia, kwa mara ya kwanza, France, ambao ni Wenyeji wa Mashindano haya, watashiriki Mechi za Makundi, wakiwa Kundi I, lakini wao hawatapewa Pointi na Mechi zao zitahesabika kama za Kirafiki tu.
Timu mbili za juu toka kila Kundi pamoja na Timu moja Bora iliyoshika Nafasi ya 3 kwenye Makundi zitatinga Fainali na Timu 8 zilizobaki ambazo zitamaliza Nafasi ya Tatu zitapangiwa Mechi maalum za Mchujo ili kupata Timu 4 za mwisho kuingia Fainali.
Mechi za Makundi zitaanza Septemba 2014 hadi Oktoba 2015 na Ratiba kamili itatolewa na UEFA baada ya Droo.


Fainali za UEFA EURO 2016 zitachezwa Nchini Ufaransa kuanzia Juni 10, 2016 hadi Julai 10, 2016 na kwa mara ya kwanza Fainali hizo zitakuwa na Nchi 24 badala ya zile 16 za kawaida.

MAKUNDI:
KUNDI A: Netherlands, Czech Republic, Turkey, Latvia, Iceland, Kazakhstan.
KUNDI B: Bosnia-Hercegovina, Belgium, Israel, Wales, Cyprus, Andorra.
KUNDI C: Spain, Ukraine, Slovakia, Belarus, FYR Macedonia, Luxembourg.
KUNDI D: Germany, Republic of Ireland, Poland, Scotland, Georgia, Gibraltar.
KUNDI E: England, Switzerland, Slovenia, Estonia, Lithuania, San Marino.
KUNDI F: Greece, Hungary, Romania, Finland, Northern Ireland, Faroe Islands.
KUNDI G: Russia, Sweden, Austria, Montenegro, Moldova, Liechtenstein.
KUNDI H: Italy, Croatia, Norway, Bulgaria, Azerbaijan, Malta.
KUNDI I: Portugal, Denmark, Serbia, Armenia, Albania.

No comments

Powered by Blogger.