Header Ads

Pamoja na zaidi ya milioni kuwa kwenye hatari, Kenya inajiandaa kukabili njaa kubwa

Wakina mama kutoka vijijini katika kaunti ya Turkana katikati wakipanga foleni kupokea msaada wa chakula kutoka kwa serikali hapo

Kutokana na hali ya ukame mkali iliyorekodiwa katika kaunti 11 na watu zaidi ya milioni kuwa katika hatari ya kukabiliwa na njaa, serikali ya Kenya imeshaanza kuchukua hatua kabla ya ukame mkali.
Mamlaka ya Taifa ya Udhibiti wa Ukame (NDMA) yaiweka serikali kwenye tahadhari, ikilenga kwenye kaunti katika mikoa ya mashariki, kaskazini, na pwani.
Mwenyekiti wa Bodi ya NDMA Agnes Ndetei aliiambia Sabahi tahadhari imeshamiri zaidi baada ya kufuatilia na kufanya tahmini ya hali iliyojionyesha katika kaunti 11 -- Marsabit, Turkana, Tana River, Garissa, Mandera, Wajir, Isiolo, Pokot Magharibi, Baringo, Samburu na Lamu -- tunashughulikia hali ya ukame.
"Baadhi ya kaunti hizi tayari zinakabiliwa na uhaba mkubwa wa maji na malisho," alisema, akiongezea kwamba kaunti nyingine 13 pia ziko katika hatari ya ukame kama msimu mrefu wa mvua hautatokea mwezi Aprili. "Tumeitaka serikali kuanza mara moja kutekeleza hatua za kupunguza kwa ajili ya jamii."


Wakaazi wa Wajir wakipita kwenye mizoga ya mifugo, huko Athibohol, kaskazini mashariki mwa Nairobi. Serikali ya Kenya inachukua hatua za tahadhari kuepuka marudio ya ukame.

"Msichana mwenye umri wa miaka 8 alifariki dunia kwa sababu ya njaa na familia ilichinja na kula mbwa katika kijiji cha Nayanae-emeyan huko Turkana tarehe 17 Januari. Matukio haya ya bahati mbaya yanatoa wito wa kuongeza kasi ya kuingilia kati kuwasaidia jamii," Ndetei alisema. "Mwitikio wa haraka na kwa bidii ni muhimu kuzuia matukio kama hayo."
Kwa mujibu wa mbunge wa Turkana Kaskazini Christopher Nakuleu, watu wanane wameishafariki dunia kwa sababu ya njaa kutoka mwezi Desemba, ikiwa ni pamoja na watoto wanne na wakina mama watu wazima wawili.
"Dazeni za watoto wenye utapiamlo wamekuwa wakihudhuria katika hospitali mbalimbali," aliiambia Sabahi.
Mwaka 2011, zaidi ya watu 40 walikufa katika Kaunti ya Turkana pekee, alisema.
Waziri wa Utoaji Madaraka na Mipango Ann Waiguru alisema watu zaidi ya milioni moja nchini yote Kenya wanakabiliwa na njaa kwa sababu ya ukame ulioenea.
Alisema serikali imechukua hatua zote muhimu kushughulikia hali hiyo, ikiwa ni pamoja na kutoa msaada wa chakula kwa kaunti za Turkana na Marsabit, ambako mahitaji ni makubwa. mpango wa Chakula Duniani unatoa msaada wa chakula kwa watu karibia milioni1, alisema.
"Tunashirikiana na viongozi wa kaunti ambazo zimebainika kuzuia vifo vyovyote," Waiguru aliiambia Sabahi.
Serikali itachukua hatua kuhakikisha hakutakuwa na marudio ya 2011, Waiguru alisema, akiongeza kwamba mipango ya muda mrefu ya serikali ya taifa na ya kaunti inajumuisha kusaidia umwagiliaji na miradi ya maji katika mikoa inayokumbwa na ukame. Serikali yajiandaa kununua mifugo
Zaidi ya hayo, serikali imeielekeza Tume ya Nyama ya Kenya kutoa kipaumbele cha kununua mifugo kutoka katika maeneo yaliyoathirika ili kusaidia kupunguza hasara yoyote wanayoweza kuipata wakulima, Katibu Mkuu wa Mifugo Khadijah Kassachoon aliiambia Sabahi.
Hadi kufikia sasa, wafugaji wanapaswa kuanza kuuza baadhi ya mifugo yao ili kuwa na mifugo wanayoimudu na kuepuka hasara kubwa, alisema, akiongeza kwamba serikali itabainisha vituo vya kununulia ambapo wakulima wanaweza kupeleka mifugo yao kuiuzia serikali.
Mwenyekiti wa Baraza la Masoko ya Mifugo la Kenya huko Garissa Ahmed Hassan alisema kama serikali itaweka bei nzuri, wakulima watakuwa na mwelekeo zaidi wa kuuza mifugo yao ili kubakia na kundi wanalolimudu, idadi ambayo inategemea uwezo wa kila mkulima na ukubwa wa ukame.
"Kuna wafugaji ambao wanaweza kuwa na wanyama 200 na wanaweza kuamua kutowauza kwa serikali," aliiambia Sabahi. "Wakati wa ukame wa mwaka 2011, serikali ilikuwa ikinunua kwa chini ya nusu ya bei na mnyama anatakiwa kuuzwa. Hilo liliwakatisha tamaa wafugaji kuuza kwa serikali na matokeo yake wanyama walikufa."
"Tunaelewa kwamba baadhi ya wafugaji watapinga kuuza wanyama wao waliowaficha kwa sababu wanahusisha idadi kubwa ya wanyama na hali ya utajiri. Lakini itakuwa vigumu kwa wamiliki kuendelea kung'ang'ania wanyama kama mvua hazitanyesha," alisema Kassachoon, akiongeza kwamba serikali bado haijapanga bei ya kununulia.
"Tunahitaji kupata wanyama hao sasa, wakati afya zao na miili yao bado ina hali nzuri, ili kupunguza msongo wa mawazo kwa malisho na maeneo ya kunyweshea mifugo yaliyopungua katika maeneo yaliyoathiriwa," alisema.
Fedha kwa ajili ya dharura ya ukame kutolewa
Katibu wa Hazina Henry Rotich aliiambia Sabahi kwamba serikali itatoa hivi karibuni takriban shilingi bilioni 3 (dola milioni 35) katika fedha za dharura ya ukame ili kusaidia kaunti zilizoathirika.
"Fedha zilitengwa kutoka katika mapato ya taifa kwa ajili ya kukabiliana na dharura kama vile ukame," aliiambia Sabahi.
Kabla ya kutolewa kwa fedha hizo, mamlaka katika Kaunti ya Wajir zilisema walikuwa wakifanya kazi wakiwa na uhaba wa rasilimali kuwasaidia wananchi juu ya ukame.
Mtendaji wa huduma ya maji wa Kaunti ya Wajir Yussuf Abdi Gedi alisema serikali ya kaunti imekuwa ikisafirisha maji kwa makazi 150.
"Hali ni mbaya [sana] kiasi kwamba baadhi ya wananchi wamekwenda katika viunga vya karibu vya Ethiopia kutafuta maji na maeneo ya kulishia," aliiambia Sabahi. "Maji ambayo yameletwa kwao yanatolewa bure kwa sababu wengi kati yao hawawezi kununua bidhaa hiyo."

Alisema visima vitatu tayari vinatumika huko Wajir na vingine 10 vimepangwa kuanza kutumika mwezi Machi

No comments

Powered by Blogger.