Header Ads

BARCA YAKALISHWA NA VALENCIA

REKODI ya kutofungwa ya Barcelona usiku huu imekomea kwenye mechi ya 31, baada ya kufungwa mabao 3-2 na Valencia.
Mabao ya Barca yalifungwa na Alexis dakika ya saba na Messi kwa penalti dakika ya 51, wakati mabao ya Valencia yalifungwa na Parejo dakika ya 44, Piatti dakika ya 46 na Alcacer dakika ya 58.

Matokeo hayo yanatoa nafasi kwa Barca kuipisha Real Madrid kileleni, kwani inabaki na pointi zake 54 sawa na Atletico Madrid, ikiwa imecheza mechi moja zaidi. Real ina pointi 53 na imecheza mechi 21, wakati Barca 22.
Ushindi wa kushitua: Wachezaji wa Valencia wakishangilia baada ya kupata bao la tatu kupitia kwa Alcacer dakika ya 58.
                      Lionel Messi akisikitika baada ya Barcelona kufungwa

No comments

Powered by Blogger.