YAKIWA YAMEBAKI MASAA MACHACHE KABLA DIRISHA LA USAJIL KUFUNGWA I: ANGALIA USAJILI ULIOKAMILIKA
Kim Kallstrom amekamilisha upimaji wa afya wa kujiunga na mkopo na
Arsenal akitokea Spartak Moscow - wakati huo huo uhamisho wa mchezaji
mkongwe wa kijerumani Miloslave Klose kuja Emirates umeshindikana
rasmi.
Uhamisho
wa beki Eliaqum Mangala na mwenzie Fernando kutoka umekwamba na
wachezaji hao wameonekana kwenye ndege wakielekea jijini Madeira kwa
ajili ya mechi ya Ligi ya Ureno kesho.
Papiss
Cisse amekataa kujiunga na klabu ya Uturuki Trabzonspor lakini msenegal
huyo bado anaweza kuuzwa usiku huu ikipatikana ofa ambayo Newcastle
wanaitaka.
Borussia Monchengladbach bado wanamhitaji mshambuliaji wa Newcastle
Chelsea
wamethibitisha kumsajili Kurt Zouma kutoka St Etienne, lakini mlinzi
huyo ataendelea kubakia kwenye timu hiyo ya Ufaransa mpaka mwisho mwa
msimu.
Kinda hilo lenye miaka 19 amejiunga na Chelsea kwa mkataba wa miaka mitano na nusu.
No comments