Header Ads

SPIKA WA BUNGE MH. MAKINDA ALIPOTEMBELEA MAKAZI YA BALOZI WETU GENEVA

 Mh. Spika Anne Makinda akishukuru baada ya kukabidhiwa  nakala ya 
Katiba ya Jumuiya ya Watanzania
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Anne Makinda ametembelea makazi ya Balozi wa Tanzania katika Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Geneva,  Mhe. Modest Mero, kumsalimu na pia kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Jumuiya ya watanzania waishio  Uswisi. Mh. Spika pamoja na ujumbe wake alikuwa Geneva, 27-28 Januari 2014, kuhudhulia kikao cha kwanza cha kamati ya Maspika kwa ajili ya kuandaa mkutano mkuu wa Dunia wa Maspika.
 Picha ya pamoja, Mh. Modet Mero, Mh. Anne Makinda na mama Mero, 
kwenya makazi ya balozi.
Mh. Spika katika picha ya pamoja na Mh. Balozi Modest Mero na 
 viongozi wa Jumuiya ya Watanzania waishio Uswisi.

No comments

Powered by Blogger.