LIVERPOOL YAJA VIZURI NA KILIO KWA EVERTON, YAIFUMUA 4-0
LIVERPOOL
imefanya maangamizi kwa majirani zao Everton baada ya kuitandika bila
huruma bao 4-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza.
Licha
ya kukosa penalti katika mchezo huo, mshambuliaji Daniel Sturridge
aling’ara na kutupia wavuni magoli mawili katika dakika ya 33 na 35.
Mshambuliaji
huyo wa Unigereza alikosa penalti kipindi cha pili na hapo hapo
akapelekwa benchi na nafasi yake kuchukuliwa na Moses.
Huu unakuwa ni ushindi mkuwa wa Liverpool dhidi ya watani wao wa jadi tangu mwaka 1982.
Bao la kwanza lilifungwa na Steven Gerrard adkika ya 21 wakati lile la mwisho lilifungwa na Suarez.
Suarez
amefunika rekodi yake ya msimu uliopita ambao alifunga magoli 23 katika
michezo 33 huku msimu huu akiwa tayari kishatupia wavuni mabao hayo
katika michezo 18 tu,
Liverpool (4-3-3)
- Mignolet 7; Flanagan 7 (Kelly 73), Skrtel 7, Toure 7, Cissokho 6;
Henderson 6, Gerrard 8, Coutinho 8 (Alberto 79); Sterling 7, Sturridge 8
(Moses 71), Suarez 7.
Everton (4-2-3-1)
- Howard 7; Stones 7, Alcaraz 5, Jagielka 6, Baines 6; McCarthy 6,
Barry 7; Mirallas 7, Barkley 7 (McGeady 76), Pienaar 5 (Osman 46, 6);
Lukaku 6 (Naismith 25, 6).
No comments