HALI SI SHWARI DRC CONGO, 20 WAFARIKI KWENYE MLIPUKO... Soma zaidi hapa
Watu 20 wanahofiwa kufariki kutokana na mlipuko katika ghala la silaha huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Vikosi
vya kulinda amani vya umoja wa mataifa nchini humo ,vimesema kuwa nyumba
nyingi zilaharibiwa wakati wa mlipuko huo katika kambi moja ya kijeshi
karibu na soko kuu la Mbuji-mayi.
Mlipuko huo uliotokea katika mji wa Mbuji-Mayi inasemekana ulisababishwa na radi
Kwa
mujibu wa taarifa za kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa
Monusco,zaidi ya watu 50 pia walijeruhiwa huku nyumba kadhaa
zikiharibiwa.
Lengo la
Monusco nchini humo ni kupokonya makundi yanayopigana silaha. DRC
inajaribu kutokamana na vita vilivyosababisha mamilioni ya vifo kati ya
mwaka 1998 na 2003.
'Nimewaamrisha
maafisa wetu walio mjini Mbuji-Mayi kushirikiana na wenyeji ili
kusaidiana kukabiliana na hali,'' alisema Martin Koble mkuu wa kikosi
hicho cha Monusco.
Mbuji-Mayi ni mji wa tatu kwa ukubwa DRC, na ndio kitovu cha uchimbaji wa madini ya Almasi.
No comments