Header Ads

AUWAWA KWA BAADA YA KUPIGWA RISASI NA MAJAMBAZI.

Wakati raia wa nchi mbalimbali wakijiandaa kwenda kutazama kombe la dunia nchini Brazil,bado vitendo vya uhalifu vinaendelea kuitikisa nchi hiyo ambapo raia mmoja aliyetambulika  kwa jina la "Yeremia José Vicente" wakati akirudi nyumbani kwake baada ya pirikapirika za hapa na pale huko Toritama, Pernambuco - Brazil, akiwa njiani ghafla majambazi yenye silaha wakiwa na pikipiki walimvamia na kumpiga risasi tatu,lakini risasi moja ndiyo iliyompata maeneo ya kichwani na kumsababishia majeraha makubwa yaliyopelekea damu nyingi kuvuja kutokana na ubongo wake kuharibiwa vibaya na risasi hiyo.


Mauaji mengine ya aina hiyo yalitokea saa chache kabla katika Manispaa ndogo ya Jimbo la Pernambuco, na majambazi haohao ndio waliohusika.


        maehemu Yeremia José Vicente
Wahalifu wengi nchini Brazil mara nyingi hufanya uhalifu wao bila kuvaa kikinga uso {mask} yoyote, hivyo ili kulinda wasijulikane Wahalifu wengi huua watu wanaowaibia, inakadiriwa kuwa wahalifu hao huwa wanauwa watu wasiopungua elfu sitini kwa mwaka na mpaka leo bado hawajapatikana.



                          Polisi wakichunguza chanzo cha tukio hili

No comments

Powered by Blogger.