Header Ads

Kesi ya Scorpion Yapigwa Kalenda

Kesi ya unyang'anyi wa kutumia silaha inayomkabili Salum Njwete ‘Scorpion’ imeahirishwa hadi Novemba 16, mwaka huu itakapotajwa tena.

Kesi hiyo iliyopo Mahakama ya Wilaya ya Ilala, imeahirishwa na Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo,  Flora Haule baada ya upande wa mashtaka kudai mahakamani hapo kuwa upelelezi wa shauri hilo  bado haujakamilika.

“Mheshimiwa Hakimu, mshtakiwa yupo mbele ya mahakama yako ila tunaomba tarehe nyingine ya kutajwa kwa sababu upelelezi wa kesi hii bado haujakamilika"alidai Wakili wa Serikali Chesensi Gavyole.

Kutokana na maombi hayo,  Hakimu Haule alikubaliana na kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.
Powered by Blogger.