Kesi ya CUF Dhidi ya Msajili Yapangiwa Jaji
KESI iliyofunguliwa na Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Wananchi (CUF) wakiomba mahakama imzuie Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, kuingilia masuala yanayohusu chama chao, imepangwa kusikilizwa mbele ya Jaji Sekieti Kihiyo.
Kesi hiyo ilipangiwa jaji wa kuisikiliza jana Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na kupangwa kutajwa kwa mara ya kwanza Novemba 10.
Katika kesi hiyo iliyopewa namba 23/2016, mbali na msajili, wadaiwa wengine ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Profesa Ibrahim Lipumba na wanachama wengine 11 wa chama hicho.
Kesi hiyo ilifunguliwa chini ya hati ya dharura na jopo la mawakili watatu; Juma Nassoro, Twaha Taslima na Hashim Mziray.
Bodi hiyo kwa niaba ya CUF, katika kesi ya msingi wanaiomba Mahakama Kuu mambo matatu, ikiwamo kutengua barua ya msajili, ya Septemba 23, mwaka huu, iliyotengua uamuzi halali wa kikao cha chama hicho.
Jambo la pili, CUF inaomba mahakama kumzuia msajili asiendelee kufuatilia suala la kufutwa kwa uanachama wa Profesa Lipumba.
Hoja ya tatu, CUF wanaomba msajili azuiliwe kuingilia masuala yanayohusu chama hicho na asimamie na kuangalia usajili wa vyama vya siasa.
Awali Jaji Mutungi alitoa hoja 11 za kumrejesha katika wadhifa wake wa uenyekiti, Profesa Lipumba.
Mbali ya Lipumba, viongozi wengine ambao msimamo wa msajili unawarejesha madarakani moja kwa moja baada ya kusimamishwa na Baraza Kuu la Uongozi la CUF, katika kikao chake cha Agosti 30, mwaka huu, kilichofanyika Dar es Salaam, ni Naibu Katibu Mkuu Bara, Magdalena Sakaya ambaye pia ni Mbunge wa Kaliua na Naibu Mkurugenzi wa Habari Taifa, Abdul Kambaya.
Wengine ni Mbunge wa Mtwara, Maftaha Nachuma, wajumbe wa Baraza Kuu Taifa; Masudi Omari Mhina, Thomas Malima, Ashura Mustafa na Kapasha Kapasha. Wamo pia Musa Haji Kombo, Habibu Mnyaa na Haroub Shamis ambao wataendelea kuhesabika kama wanachama halali wa chama hicho.
Katika barua yake kwa viongozi wa CUF, msajili alieleza kuwa amefikia msimamo wake huo baada ya kupata nafasi ya kusikiliza pande zote zinazosigana katika mgogoro huo wa uongozi ndani ya chama hicho.
Alisema katika kufikia maamuzi hayo, amezingatia mamlaka na wajibu wa msajili kushughulikia mgogoro huo, hoja za kujiuzulu kwa Profesa Lipumba, Profesa Lipumba kutengua barua yake ya kujiuzulu, uhalali wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CUF wa Agosti 21, mwaka huu na baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu kuhitaji Profesa Lipumba aitwe katika chumba cha mkutano kujieleza.
Hija nyingine ni uhalali wa kura zilizopigwa kukubali au kukataa Profesa Lipumba kujiuzulu, uhalali wa kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Agosti 28, mwaka huu, utaratibu wa kuchukua hatua za kinidhamu, uhalali wa kamati iliyoundwa na Baraza Kuu la Uongozi la Agosti 28 ili kufanya kazi ya mwenyekiti na makamu mwenyekiti wa taifa na mwisho ni kuhusu uhalali wa uteuzi wa viongozi wa kitaifa uliofanywa na kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa cha Agosti 28, mwaka huu.
Credit: Mtanzania