Header Ads

Waziri Nape: Marufuku Simba na Yanga Kutumia Uwanja wa Taifa

Baada ya mashabiki wa Simba kuvunja viti vya uwanja wa taifa katika mchezo wa Simba na Yanga uliopigwa  Jumamosi na kumalizika kwa sare ya goli ya moja kwa moja, serikali kupitia kwa Waziri wa Michezo, Nape Nnauye Imepiga marufuku uwanja wa taifa kutumika na timu za Yanga na Simba.

Waziri Nape amefanya maamuzi hayo baada ya jana Jumapili kufanya ziara katika uwanja wa taifa kushuhudia uharibifu wa viti uliotokea juzi Jumamosi .

Amesema kutokana na tukio ambalo limejitokeza, kuanzia sasa michezo ya timu hizo haitaruhusiwa kufanyika katika uwanja huo hadi pale ambapo serikali itawaruhusu.
“Uwanja huu hautatumika kwa Yanga na Simba mpaka pale tutakapoamua vinginevyo hapo baadae, hawatatumia uwanja huu watafute viwanja vingine, sababu hapa kuna pesa za walipa kodi, kuna pesa za watanzania.

“Wanaotakiwa kutumia uwanja huu ukiwa mzuri kama ulivyo ni wengi kuliko Yanga na Simba, wapo wengine ambao ni wastaarabu wanaweza kutumia uwanja huu,” aLIsema Waziri Nape.

Maamuzi mengine ni Simba kutakiwa kulipia gharama ya viti 1,781 vilivyoharibika, Simba haitapata mgao wa mchezo hadi walipe gharama za uharibifu, kamera za CCTV zitafungwa uwanja mzima na Yanga itatakiwa kulipa gharama ya mageti manne ya upande wa mashabiki wake yaliyovunjwa.

No comments

Powered by Blogger.