Header Ads

Zaidi ya waasi 150 wauawa nchini DRC Congo

Wanajeshi Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamefanikiwa kuwaua wapiganaji wa Waasi wapatao 150 katika mapigano na waasi hao kufikia hadi leo,tangu mwezi Julai haya ndo mapigano yaliyoweza kutikisa anga la watu wa Congo yakiongozwa na kundi la wapiganaji la M23 lililotangaza kuuteka mji wa Goma ambao upo Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
     
Taarifa za awali zilizothibitishwa na msemaji mkuu wa Nchi hiyo bw.Lambert Mende zinasema wapiganaji wapatao 51 waliuawa huku wakiwa wamevalia sare za jeshi la Rwanda jambo ambalo serikali ya Rwanda wamekanusha kuhusiana na tuhuma za awali zinazodai kuwa Taifa hilo linawaunga mkono waasi hao kutokuhama katika eneo hilo lenye utajiri mkubwa wa Madini.
   
Umoja wa matifa unazishutuma nchi za Rwanda na Uganda kuhusika na mapigano ya mara kwa mara ambayo mpaka leo ijumaa yanaendelea kaskazini mwa mji wa Goma katika eneo la Kibumba.Hali si shwari katika eneo hilo huku wakazi wakilazimika kuyahama makazi yao kuelekea katika vitongoji vilivyoko kaskazini magharibi mwa Goma ambako ndiko kuna kambi kubwa ya wakimbizi ya Kibai.

Lutena Kanali Prosper Basse ambaye ndiye msemaji mkuu wa kimataifa nchini Congo amesema mapigano mengine bado yanaendelea kilomita zipatazo 900 kaskazini mwa Goma.Majeshi ya Serikali ya Congo yanaendelea na mapigano na Waasi huku yakiutwaa mji wa Mabenga na kufanikiwa kusonga mbele kuelekea mji wa Kiwanja uliomaarufu kwa wapiganaji hao wa M23.

No comments

Powered by Blogger.