Rais Magufuli aweka jiwe la msingi katika daraja la waenda kwa miguu Furahisha....

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli
ameitaka Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano kuhakikisha kuwa
ujenzi wa daraja la watembea kwa miguu na upanuzi wa Barabara ya
Makongoro jijini Mwanza unakamilika ifikapo disemba mwaka huu.
Aidha amesema upanuzi wa barabara ya Makongoro uliokuwa ujengwe kati
ya Furahisha hadi Pasiansi Km 2.8 sasa utaendelezwa hadi kufikia uwanja
wa ndege.
Akizungumza
jana mara baada ya kuweka jiwe la msingi la daraja la watembea kwa
miguu na upanuzi wa barabara ya Makongoro Mh. Dkt. Magufuli alisema kasi
ya ujenzi wa barabara jijini Mwanza uendane na ujenzi wa uwanja wa
ndege ili kuwezesha mkoa wa Mwanza kuwa kitovu cha nchi za maziwa makuu.
“Nakuagiza Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano uhakikishe kuwa
barabara na daraja la watembea kwa miguu Furahisha vinakamilika mwezi
desemba na mkandarasi wa uwanja wa ndege anaanza kazi mara moja”.
Alisisitiza Rais Dkt. Magufuli.
Alisema nia ya Serikali yake ni kununua meli mbili na kujenga daraja
kati ya Kigongo na Busisi ili kuboresha huduma za usafiri katika Ziwa
Victoria.

Naye Mtendaji mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Eng.
Patrick Mfugale alimtaka mkandarasi anaejenga daraja la waenda kwa miguu
na barabara ya Makongoro kuhakikisha ujenzi wake unakamilika kwa wakati
na ubora unaotakiwa.
Zaidi ya shilingi bilioni 6.4 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi huo
utakaopunguza msongamano wa magari na ajali katika barabara ya
makongoro jijini Mw.anza.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na
Mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani, Mbunge wa Sumve Richard
Ndassa wakipiga makofi mara baada ya tukio la uwekaji wa Jiwe la Msingi
la Ujenzi wa Daraja la waenda kwa miguu la Furahisha pamoja na Upanuzi
wa barabara ya Mwanza-airport.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS, Mhandisi Patrick
Mfugale akitoa maelezo ya namna daraja la Furahisha litakavyokuwa mara
baada ya kukamilika
No comments