Manchester United wanatarajia kumtangaza Jose Mourinho kuwa kocha wake mpya..
Ikiwa United imeshindwa kufuzu kushiriki kombe la mabingwa wa Ulaya chini ya kocha wake wa sasa, Louis van Gaal, uongozi wa Old Trafford unafikiriwa kuamua kufanya mabadiliko yanayohitajika.
Mourinho amekuwa benchi tangu atimuliwe na Chelsea December mwaka jana.
Klabu hiyo imepanga kutangaza ujio wake mapema wiki ijayo baada ya kumwambia Van Gaal, 64, afungashe virago vyake.
Kocha huyo raia wa Uholanzi bado ana msimu mmoja kwenye mkataba wake wa miaka mitatu na licha ya kutumia paundi milioni 250 kusajili wachezaji wapya, ukocha wake umewaangusha mashabiki wengi kwa timu yake kumaliza katika nafasi ya nne na kisha ya tano kwenye ligi kuu ya England katika misimu miwili aliyoifundisha.
Mourinho alikuwa kwenye mchezo wa masumbwi Jumamosi hii ambapo bondia David Haye alishinda lakini alikataa kuongea chochote iwapo anaenda kumrithi Van Gaal.
Mourinho ni mmoja wa makocha waliofanikiwa zaidi huku akishinda vikombe vitatu akiwa na Chelsea, pamoja na kuingoza Porto na Inter Milan kwenye ushindi wa ligi ya mabingwa mwaka 2004 na 2010.
Aliwahi pia kuwa kocha wa Real Madrid na kuiwezesha kushinda kombe la Spanish La Liga mwaka 2012.
No comments