Dk Hamisi Kigwangalla ataja tofauti kati ya BANGI na VIROBA
Naibu Waziri wa Afya, Dk Hamisi Kigwangalla jana alitumia dakika kadhaa kutoa ufafanuzi kwa wabunge kuhusu tofauti iliyopo kati ya dawa za kulevya aina ya bangi na pombe kali za viroba.
Alisema pombe yenye kilevi kilichothibitishwa haiwezi kuathiri afya ya mtumiaji kama ilivyo dawa ya kulevya.
Ufafanuzi huo ulitokana na swali la Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya maswala ya Ukimwi,Mohammed Amour aliyetaka kujua tofauti ya kitaalamu baina ya bangi na kiroba kutokana na jinsi zinavyowatesa watumiaji.
Mbunge huyo wa Bumbwini Unguja alisema kuna kiwango kikubwa cha kilevi kilichopo katika viroba kinachoweza kusababisha athari kwa watumiaji.
Akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo kwenye ofisi ya wakala wa maabara ya mkemia mkuu wa serikali, Dr. Kigwangalla alisema: "Madhara yanatofautina, ya muda mrefu na ya muda mfupi.Utumiaji wa bangi unaathiri mfumo wa fahamu kwenye ubongo, lakini pombe iliyopimwa kiasi cha alkoholi haiwezi kukuathiri."
Licha ya majibu hayo,Dr. Kigwangalla aliahidi kufuatilia suala hilo katika mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) ambayo inahusika na vipimo kutokana na udanganyifu unaofanywa na baadhi ya wafanyabiashara.
"Nitafuatilia kwa kina TFDA nione wanafanyaje, kwa nini viroba vimekuwa vikiuzwa mitaani tofauti na viwango halisi vya alkoholi." Alisema
Awali, Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele alisema wafanyabiashara wa viroba wamekuwa wakitumia ujanja wa kuweka nembo ya asilimia ndogo lakini uhalisia wa kiwango cha alkoholi katika kiroba chenyewe ni kikubwa zaidi.
“Wanabandika asilimia sita kumbe ni asilimia hata 30 ya alkoholi.”

No comments