Rais Magufuli amtembelea na kumfariji mama Maria Nyerere kufuatia kufiwa na mkwewe Bi Leticia Nyerere
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe
11 Januari, 2016 amemtembelea na kumpa pole mke wa Baba wa Taifa, Mama
Maria Nyerere kufuatia kifo cha Mkwewe Leticia Nyerere kilichotokea jana
huko Maryland Marekani alikopelekwa kwa ajili ya kupata matibabu mapema
mwezi huu.
Pamoja
na kutoa mkono wa pole kwa Mama Maria Nyerere nyumbani kwake Msasani
Jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli pia amewapa pole wanafamilia
wote na amewaomba kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu cha
kuondokewa na ndugu yao.
Msemaji wa familia ya Mwalimu Nyerere Bwana Joseph Butiku amemueleza Rais Magufuli kuwa familia inaendelea na taratibu za kuusafirisha mwili wa marehemu kutoka nchini Marekani na itatoa taarifa baadaye.
Msemaji wa familia ya Mwalimu Nyerere Bwana Joseph Butiku amemueleza Rais Magufuli kuwa familia inaendelea na taratibu za kuusafirisha mwili wa marehemu kutoka nchini Marekani na itatoa taarifa baadaye.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
11 Januari, 2016
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
11 Januari, 2016
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole
Mama Maria Nyerere kufatia kufiwa na Mkwe wake Bi Leticia Nyerere
aliyefariki huko nchini Marekani. Rais alikwenda nyumbani kwa Baba wa
Taifa Msasani Dar es salaam kumpa pole Mama nyerere Januari 11,2016
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapa
pole wanafamilia alipofika nyumbani kwa Baba wa Taifa Msasani Dar es
salaam kumpa pole Mama nyerere Januari 11,2016
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipata maelezo juu ya uataratibu wa msiba kutoka kwa mwanafamilia Joseph Butiku
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja na wanafamilia
Rais
Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiagana na Mama Maria Nyerere, Mjane wa
Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, na wanafamilia
alipokwenda nyumbani kwake Msasani kumfariji kufuatia kifo cha Mkwe wake
Marehemu Leticia Nyerere huko Maryland, Marekani.
No comments