Header Ads

Onyo kali kwa madaktari wanaotoa mimba...

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaonya Madaktari vinara wa Hospitali ya Rufaa ya Songea ambao wanasifika kwa kufanya biashara ya kutoa mimba wanawake na wanafunzi kuacha tabia mara moja,lasivyo  atawafukuza kazi na kuwafunga jela.

Waziri Mkuu alitoa onyo hilo jana wakati alipotembelea Hospitali hiyo na kuzungumza na watumishi kwa lengo la kuwasisitiza kutoa huduma bora kwa wagonjwa,ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku 3 mkoani Ruvuma.

Alisema Hospitali ya mkoa huo inasifika kwa kutoa mimba wanawake na kuwalaza wagonjwa wao wodi namba 5, kitendo ambacho serikali haikuruhusu wala haikubaliani nacho.

"Naomba mkuu wa mkoa fanya ziara ya kushtukiza katika wodi namba 5 utakuta wanawake wametolewa mimba, wakiwemo wanafunzi na kisha madaktati hao wanatumia wodi zetu kuwalaza wagonjwa wao waliowatoa mimba.Ni marufuku na nitawachukulia hatua kwani majina ya madaktari hao ninayo," alisisitiza majaliwa.

Waziri Mkuu Majaliwa alimuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa huo,Dr. Daniel Malekela na Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Dr. Phils Nyimbi kuwafuatilia madaktari wanaojihusisha na vitendo hivyo na kutoa taarifa ili wachukuliwe hatua kali.

Pia, alimuagiza mganga mkuu Dkt Daniel Malekela kuondoa duka lake lililo jirani na hospitali hiyo ili kuondo hisia kwamba dawa zinaibiwa na kupelekwa kwenye maduka ya watumishi.

No comments

Powered by Blogger.