Header Ads

Breaking News.. CHADEMA yapata pigo zito baada ya Juma Haji ajitoa rasmi katika....

Hizi ni taarifa za uhakika nilizopata kutoka kwa chanzo muhimu kilicho jirani na Mwanasiasa Mkongwe, Juma Duni Haji ambaye aliamua kujivua uanachama wake wa CUF na kujiunga na CHADEMA kutokana na tamaa ya kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Babu Duni baada ya kujiunga na CHADEMA aliteuliwa kuwa Mgombea Mwenza akisaidiana na Edward Lowasa katika kampeni za kuelekea Magogoni.

Baada ya uchaguzi Mkuu ambapo CCM kupitia Mgombea Urais wake John Pombe Magufuli ilishinda uchaguzi huo huku ikinyakua viti vya kutosha kwa upande wa Wabunge na Udiwani. Matokeo hayo yalimuondoa Babu Duni kwenye siasa za Tanzania. Tangu wakati huo, hajasikika akikubali ushindi ama kukataa. Kitendo hicho cha kukaa kimya kimetafsiriwa kwa hisia tofauti. Wapo wanaodai kuwa Juma Duni amerejea CUF huku wengine wakimnukuu akisema kuwa atatoa hatma yake kisiasa ifikapo Januari Mwakani.

Kamera yangu ilizama Zanzibar ili kufuatilia nyenendo za mwanasiasa huyo na kutaka kujua juu ya ukimya wake. Kwa hakika niliyoyakuta ni hatareeeeee! Kwa kifupi Juma Duni Haji hayupo CHADEMA. Kamera yangu imenyaka sababu za mwanasiasa huyo kujiengua CHADEMA.

1. Kutolipwa madai yake ya shilingi milioni 200. Kama mnavyofahamu kuwa Juma Duni Haji aliahidiwa kitita cha shilingi milioni 550 ikiwa ataondoka CUF na kujiunga na CHADEMA. Baada tu ya kujiunga, Babu Duni alipata milioni 50 na aliahidiwa kiasi kingine angepewa kabla ya kampeni kumalizika. Mwezi mmoja baada ya kampeni, Babu Duni akaanzisha mgomo kwa lengo la kushinikiza alipwe kiasi anachodai ambacho ni milioni 500. Akaacha kushiriki mikutano ya kampeni. CHADEMA kupitia mgombea wao wa Urais wakaona jahazi linazama. Wakazama mfukoni na kumpa milioni 300 fedha ambazo zilitolewa na mmoja wa wafanyabiashara waliokuwa wanaunga mkono UKAWA. Kiasi cha shilingi milioni 200 zilizobaki walimuahidi kumlipa wiki moja kabla ya uchaguzi. Hata hivyo, mpaka sasa, Babu Duni hajalipwa fedha hizo na ndo maana ameamua kujiondoa CHADEMA.

2. Kukatika kwa mawasiliano na viongozi waandamizi wa CHADEMA na UKAWA. Babu Duni amesikika akilalamika kuwa hajapigiwa simu ama kuwa na mawaziliano ya ana kwa ana na viongozi waandamizi wa chama chake cha CHADEMA na UKAWA licha ya jitihada ambazo amekuwa akizifanya. Kwamba, kila anapowasiliana na viongozi wenzake, wanamjibu kuwa watampigia lakini wamekuwa hawafanyi hivyo. Anamshangaa hata Lowasa kwa kitendo chake cha kukaa kimya ilhali waliongea mengi na walipanga mikakati mingi ya maisha baada ya uchaguzi lakini hakuna kinachoendelea.

3. Vijembe na kejeli kutoka kwa makada wa CUF. Babu duni amesikika akilalama kuwa anapewa vijembe na viongozi na wafuasi wa CUF kwa kitendo chake cha kukisaliti chama hicho na kujiunga na CHADEMA. Anasema kuwa CUF inamuona kama ni msaliti na kwamba uamuzi wa yeye kwenda CHADEMA ulifanywa na Maalim Seif Sharif Hamad pekee.

Kutokana na sababu hizi na nyingine nyingi, Babu Duni anasema kuwa haoni umuhimu wa kuendelea kubaki CHADEMA. Anasema kwa sasa anaendelea kutafakari na soon atatoa hatma yake kisiasa. Anasema kuwa kuna mambo mawili anayatafakari. Ama kurejea CUF na kuendelea maisha ya kisiasa ama kustaafu siasa. Tusubiri tuone.

Nawasilisha


Chanzo: JF

No comments

Powered by Blogger.