Header Ads

Sitta: Sifa zote za kuongoza Bunge lijalo ninazo

Dar es Salaam. Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Samuel Sitta amesema kutokana na hali ya joto la kisiasa ilivyo, ambayo ilidhihirika zaidi wakati wa uchaguzi, wabunge walioshinda wengi ni vijana na ni wazi spika anayehitajika ni mwenye uzoefu.

Sitta ameyasema hayo leo wakati akihojiwa na Radio Uhuru FM, ambako amethibisisha kwamba naye anakusudia kugombea nafasi hiyo ya uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuwa anaamini anazo sifa zote zinazohitajika.

Sitta ambaye amewahi kuwa Spika wa Bunge la tisa,Mwenyekiti wa Bunge la Katiba amesema licha ya kwamba wapo waliojaribu kumshawishi asigombee nafasi hiyo tena, badala yake awe anatoa ushauri pale inapobidi, amesisitiza bado ana wito wa kuwatumikia wananchi kwa njia hiyo.

“ Ili Bunge lisiwe uwanja wa malumbano, liwe la maslahi ya wananchi Spika anayestahili ni mwenye uwezo wa kuvumilia na anayezijua vyema kanuni za Bunge, nina sifa hizo nitagombea, nikishinda nitahakikisha ninawakusanya wabunge wote ili wafanye kazi kwa maslahi ya nchi yaani watawaliwe na uzalendo zaidi,” alisema.

Alisisitiza kuwa pia anatambua kiu iliyopo sasa ni kupata katiba mpya, hivyo Bunge linajukumu la kutunga sheria iwapo katiba inayopendekezwa , hivyo ni lazima liwe na spika makini ambaye atasaidia katika kuwezesha sheria madhubuti kupatikana.

No comments

Powered by Blogger.