Kasi ya Magufuli yazidi kuwaweka watendaji wa serekali roho juu
Katika kile kinachoonekana ni kutaka kwenda na kasi ya rais wa awamu ya tano, Dk. John Magufuli, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Rada kata ya Majohe, Jimbo la Ukonga, Abdallah Goma, amewatimua ofisini wajumbe watano wa mtaa na kuwataka waende mitaani kukusanya kero zinazowakabili wananchi.
Mwenyekiti huyo aliamua kuchukua hatua hiyo baada ya wananchi kulalamikia tabia ya wajumbe hao kuwadai malipo wakati wanapokwenda kutaka huduma katika ofisi hiyo, ikiwamo kuandikiwa barua ya utambulisho benki.
Goma aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na Nipashe jijini Dar es Salaam jana kutokana na mvutano uliojitokeza kati yake na wajumbe aliowatimua kugoma kutekeleza agizo lake na kususia vikao.
Alisema baada ya kuapishwa alipanga ratiba ya kila mjumbe kukaa ofisini kwa muda wa siku mbili, lengo likiwa ni kubaini tabia zao, hivyo katika kipindi hicho malalamiko ya lugha chafu, kudai malipo ya kuandika barua ya dhamana na utambulisho yalijitokeza. Tumeamua kutoa huduma bure au kwa kuchangia gharama kidogo ya uchapishaji lakini siyo lazima ikiwa mwananchi hawezi kuchangia, alisema. Alisema wajumbe waliruhusiwa kukaa ofisini kabla ya serikali kuajiri Afisa Mtendaji wa Mtaa, lakini kwasababu mtendaji ameshaajiriwa kazi ya wajumbe hao ni kukusanya kero tu.
Mmoja wa wajumbe hao, Siwema Makamba, alisema wao wanajitambua kuwa ni wajumbe halali waliochaguliwa na wananchi na ni wajibu wao kuwatumikia kwa nguvu zao zote.
Alisema kitendo cha Mwenyekiti kuwafukuza ofisini ni kuwadhalilisha ili yeye atumie fursa hiyo kurudisha pesa zake alizotumia kwenye uchaguzi na kwamba siyo haki kwa wao kwenda kuzunguka mitaani.
Changamoto ya ofisi ymtaa ni kutokuwa na mawasiliano mazuri na kusababisha mvutano wetu na mwenyekiti, tunapaswa kuondoa tafauti ili tufanye kazi za wananchi, alisema.
Mmoja wa wakazi wa mtaa wa Rada, Maulid Janga alisema yeye amesikitishwa na kitendo cha wajumbe kumlipisha Sh. 50,000 kwa ajili ya kuliinua baraza la mtaa kwenda kushughulikia mgogoro wa mpaka.
Unajua hadi leo mgogoro wa mpaka haujashughulikiwa na pesa zimeliwa hivi hivi na wajanja, kama walijua hawawezi kutatua tatizo kwanini wachukue fedha zangu, alisema kwa masikitiko.
Afisa Mtendaji wa kata ya Majohe Serrda Chidaga, alisema yeye ameshangazwa na mvutano wa wajumbe kungíangíania kukaa ofisini na kushindwa kwenda mtaani kukusanya kero za wananchi.Baraza la maendeleo la kata (WDC) limekaa na kujadili suala hilo na kutoa maelekezo kuwa hawatakiwi kukaa ofisini lakini nashangaa bado wanangíangíania, lazima hatua za kinidhamu zichukuliwe ikibainika kuna maslahi binafsi,î alisema.

No comments