Header Ads

Chuo kikuu cha Kiislam kilichopo Manzese chadaiwa kuchomwa moto

Akizungumza mbele ya Mbunge wa Jimbo la Ubongo, Saed Kubenea (Chadema), mlezi wa chuo hicho ambaye pia ni diwani wa Manzese kupitia chama cha wananchi CUF, Ramadhani Kwangaya amesema moto huo uliwaka saa 2:30 usiku wa jana wakati watoto wanaosoma chuoni hapo walipokuwa wamesharuhusiwa.

Kwangaya alimwambia Kubenea kuwa inaelekea kuwa wachomaji wa chuo  hicho walikuwa ni watu walioelekezwa kwani walijaribu kuvunja dirisha la kwanza wakakuta hakina magodoro ndipo walipoenda kwenye chumba chenye magodoro na kuchoma moto .

Kwa mujibu wa Kwangaya chumba  hicho kilikuwa na magodoro 30, ambayo watoto wa chuo hicho huwa wanatumia, na sasa yameteketezwa yote.
Chuo hicho kinaendeshwa na watu mbalimbali kwa njia ya kujitolea Kufuatia hali hiyo Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea aliahidi kuchangia shilingi milioni 1, na kusema kuwa madiwani wa Jimbo la Ubungo nao walikuwa wanakusanya michango kupitia kwa diwani wa kata ya Ubungo Boniface Jacob ili waweze  kusaidia kukirejesha chuo hicho katika hali yake ya awali kiendelee kutoa huduma.

No comments

Powered by Blogger.