Header Ads

Wabunge wafunguka kuhusu kifo cha Deo Filikunjombe

Kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Ludewa mkoani Njombe, Deo Filikunjombe, simanzi, vilio na huzuni vimetanda miongoni mwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaomaliza muda wao. Wakizungumza na gazeti hili kwa simu kwa nyakati tofauti, baadhi ya wabunge wenzake, walimwelezea Filikunjombe kama mtumishi bora wa umma na hazina ya ukombozi wa wanyonge.

LUSINDE AISHIWA NGUVU
Mbunge wa Mtera, Dodoma kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Livingstone Lusinde katika rambirambi zake, alisema: “Sielewi niseme nini, nimeishiwa nguvu, Deo alikuwa kiongozi kijana, mwenye msimamo na jasiri. Alikuwa tayari kupambana na maovu bila kujali yamefanywa na chama chake au wapinzani.

KAFULILA AKUMBUKA U-BESTMAN
Naye mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR- MAGEUZI), David Kafulila alikumbuka jinsi mbunge huyo wa Ludewa alivyokubali kuwa mpambe wake wa harusi (bestman) bila kujali tofauti zao za vyama.

SERUKAMBA ABUBUJIKWA MACHOZI
Katika salamu zake za rambirambi, aliyekuwa mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba alishindwa kuzuia hisia zake na kujikuta akibubujikwa machozi ambapo pia alisema: “Huu ni msiba mkubwa, Deo alikuwa na upendo, mtu mkweli aliyekuwa tayari kulifanya tatizo la mtu mwingine kuwa lake.

MAGIGE ‘AMISS’ UPENDO WA DEO
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha, Catherine Magige alisema: “Deo alikuwa makamu mwenyekiti wetu wa PAC (Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali), alitupenda wote, tulishirikiana naye vizuri, taifa limepoteza mtu muhimu. Nitaumiss upendo wake.”

 ZITTO AKIRI KUPOTEZA RAFIKI
Naye Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe alisema: “Ndugu yetu, rafi ki yetu na mzalendo mwenzetu ametutoka.” Mungu ailaze roho ya marehemu mahalipema peponi, Amen.

No comments

Powered by Blogger.