LUBUVA - MALALAMIKO YA VYAMA YATATULIWE NDANI YA KAMATI YA MAADILI NA SIO VYOMBO VYA HABARI
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu, Damian Lubuva akizungumza katika mkutano na vyama vya siasa kujadili masuala mbalimbali kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Mkurugenzi wa uchaguzi, Kailima Ramadhan akizungumza na wadau wa vyama vya siasa leo jiji ni Dar es Salaam.
Wajumbe wa mkutano huo wakifuatilia maada leo jijini Dar es Salaam.
MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu ,Damian Lubuva amevitaka vyama vya siasa kupeleka malalamiko yao katika kamati ya maadili ya NEC na sio kwenda kutoa malalamiko yao katika vyombo vya habari.
Lubuva aliyasema hayo leo wakati NEC ilipokutana na vyama vya siasa kujadili masuala mbalimbali kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu,amesema kuwa nafasi vya siasa vina nafasi ya kuhamasisha watu wapige kura kwa wale wenye sifa.
Amesema wakati wa kupiga kura watu wakipiga kura wanatakiwa kuondoka na kazi zingine zitafanywa na mawakala ndio watakaofanya kazi zoezi la kuhesabu na baadae kubandika.
Lubuva amesema watu wakikaa vituoni wanaweza kuvuruga amani na kufanya zoezi la upigaji kura kuharibika.
Amesema tume imejipanga katika kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa uhuru na haki kutokana na mfumo wa kisasa.
Aidha amevitaka vyama vya siasa kunadi sera zao na sio kushughulika na watu kwani wananchi wanahitaji sera waweze kufanya maamuzi ya kuchagua kiongozi.
Baadhi ya vyama vya siasa vimeridhishwa na ushirikishwaji wa NEC katika masuala kuelekea uchaguzi mkuu na jinsi walivyojipanga uendeshashaji wa uchaguzi mkuu.

No comments