Njia 11 za kumtambua mpenzi wako anayekudanganya
Kila mmoja atakubaliana na mimi kwamba mahusiano baina ya wapendanao yalikusudiwa kuwa ya upendo, maelewano, kuaminiana, na urafiki wa hali ya juu, kwa bahati mbaya hali halisi siyo hiyo katika mahusiano ya wengi. Wengi wetu wameumizwa kwa mpenzi mmoja au maranyingine wote kutokuwa waaminifu katika mahusiano yao. Kutokuwa mwaminifu hapa namaanisha hali ya mpenzi mmoja kuwa na mahusiano yasiyo rasmi na mpenzi au wapenzi wengine pembeni. Japo jambo hili hufanyika kwa siri sana kwa kuogopa kuharibu mahusiano mtu aliyonayo, wako baadhi ambao wamegundulika na mahusiano yakaathirika kwa kiasi kikubwa na wengine yalikufa kabisa.
Wako ambao wameweza kuhimili machungu ya kugundua hali ya wapenzi wao kutokuwa waaminifu lakini pia wako ambao imewashinda kabisa kuwa wavumilivu, wako ambao hali hii imewaletea shida kihisia, kisaikolojia na hata kiafya. Kwa bahati mbaya wengi wetu hatuzijui hata dalili au alama zozote zakutujulisha mabadiliko waliyonayo wapenzi wetu ili basi walao tuanze mapema kufanya uchunguzi au kupeana tahadhari kabla makubwa na machungu zaidi hayajatokea. Zifuatazo nia alama zitakazokusaidia kuwamacho mara utakapoona mazingira ya kufanana nazo yanatokea katika mahusiano yenu, alama hizi nimezikusanya katika mazungumzo na baadhi ya watu niliowahi kusaidiana nao kutatua matatizo ya mahusiano yao na pia nikazihakikisha kupitia kusoma vitabu mbalimbali, kwahiyo ninauhakika zitakusaidia kuona uhalisi wa mambo, na yamkini utaona baadhi ya alama ambazo umeshawahi kuzihisi au kuzishuhudia katika mahusiano yako.
1.Kuongezeka kwa ghafla kwa hali ya kujipenda:
Yawezekana mpenzi wako alikuwa amezoea kuvaa kawaida, hapa simaanishi kutopendeza, na wewe ulikuwa umemzoea katika halifulani ya mavazi au mitindo mara ghafla anabadilika nakuwa mtanashati zaidi, ana badilisha mavazi, anapenda mavazi ya garama, labda alikuwa hatumii manukato lakini gafla anaanza kupenda manukato tena ya garama, anakuwa mtu wakujijali zaidi ya kawaida yake kiasi ambacho hukumzoea. Katika hali hii jaribu kuwa macho zaidi kufahamu nini kilicho sababisha mabadiliko ya gafla kiasi hicho.
2. Kuanza kuchelewa kutoka kazini mara kwa mara:
Sio kwamba kila mtu anapochelewa kutoka kazini basi anakuwa sio mwaminifu, lakini zaidi ya asilimia 75 (kutoka kwente tafiti) ya ambao wamekuwa na mahusiano nje wamekuwa wakitoa visingizio vinavyohusiana na kazi, vikao, mikutano na safari za kikazi, yamkini wewe ni shahidi wa hili. Unaweza kukuta mtu alikuwa anafanya kazi hiyo muda mrefu tu tangia muanze mapenzi yenu, mara gafla hali inabadilika, sikuhizi anachelewa sana kurudi nyumbani, na anaporudi unaweza kutegemea utamwona amechoka kimwili na hata kiakili kwa majukumu ya kazi kuhusiana na asili ya kazi anayoifanya lakini unakuta mtu wala haonyeshi kuchoka, anafuraha kama kawaida. Hali hii inapojitokeza mara kwa mara usichelewe kufungua macho na kudadisi mazingira maana yamkini ni kweli amepata kazi ya ziada ila siyo ile ya ajira unayoijua wewe.
3. Kupenda kutembea na mipira ya kinga mara kwa mara (condoms)
Inashangaza maranyingine kusikia mpenzi mmoja anatabia ya kubeba kondom kwenye pochi yake au mfukoni kwa kisingizio kuwa anajali, cha kushangaza zaidi unakuta yuko katika mahusiano na mkewe au mumewe. Yamkini nikweli kunakujali na labda katika mahusiano yenu hili sio la kushtua kwasababu mnajali afya zenu au mnatumia kondomu kwa sababu zaidi ya moja, lakini inakuwaje pale unapogundua kuwa ile kondom uliyokuwa unaiona haipo tena na yamkini wewe hukuhusika katika kuitumia.
4 Mazingira tatanishi ya simu:
Inawezekana mpenzi wako sio mtu wa kupokea simu au kupiga simu sana, na hivi ndiyo ulivyomzoea, mara gafla simu zinaanza kumiminika mpaka mida ya usiku. Yamkini pia alikuwa yuko huru hata simu yake inapolia waweza ichukua na kumpatia lakini gafla anakuwa na hofu kubwa na kuificha simu yake, nimeongea na wengine ambao wanakwenda na simu hadi bafuni isije ikasikika. Wengine wameanza kuondoa milio katika simu zao wakati haikuwa kawaida yao, wengine wamegundua kila mbinu ya kuweka namba ya siri (password) ngumu hadi mwenyewe anashindwa kuikumbuka wakati mwingine, wako ambao simu zao zikipigwa hawawezi kupokea na kuongea kwa uhuru kama kawaida, ataondoka na kujitenga pembeni akijifanya anaongea kiuaminifu kabisa lakini mtu uliyempenda na umkamzoea unaweza kugundua uhalisi wa anachokiongea kwenye simu na jinsia ya anayeongea naye kwa kumuangalia usoni tu. Yamkini mpenzi wako amepigiwa simu na kwasababu hakuwepo karibu ukaipokea, na mara mpigaji wa simu anapogundua aliyepokea sio mwenye simu anakata simu hiyo gafla, au gafla unagundua kila simu inayopigwa. kwenye simu ya mpenzi wako haionyeshi namba au haionyeshi jina. Mazingira kama haya yanapozidi basi jaribu kuchukuwa hatua, yawezekana kuna mvamizi tayari katika mahusiano yenu.
5.Harufu ambazo hujazizoea:
Kwa kuwa wapendanao huwa wamezoeana,maranyingi hata aina ya manukato mmoja anayotumia yanakuwa yanajulikana kwa mwenzake, hata kama mmoja hajui jina la manukato anayotumia mpenzi wake lakini basi atajua walau jinsi yanavyonukia. Sasa hembu fikiri unamkuta mpenzi wako ametokea na anaharufu ya tofauti kabisa na uliyoizoea, yamkini umeisikia harufu hiyo akiwa amerudi toka kazini wakati asubuhi alipoondoka alikuwa na harufu ile uliyoizoea. Najua hali hii inaweza kuwa na sababu zinazoeleweka lakini maranyingine ni ishara ya kuashiria kutokuwepo na uaminifu baina ya mpenzi mmoja. Maranyingine sio harufu bali michubuko katika maeneo fulani ya mwili ambayo hayana maelezo fasaha yalikotokea, iko michubuko mingine ambayo inajieleza na kutia shaka zaidi, yawezekana, ni mpenzi wa kiume lakini unamkuta na ishara za rangi ya midomo (lip sick) kwenye nguo au mwilini, sidhani kama na hapa bado maelezo yake yataingia akilini kiurahisi.
6. Tabia za kuanza kukufuatilia sana au hata kukuganda:
Nimeshawahi kuwa na mazungumzo na watu wajinsia ya kike waliokuwa kwenye mahusiano ambapo wanaume wao walikuwa hawawaachi, watawapeleka kila wanakotaka, nakutoruhusu mazingira ya wapenzi hawa wakike kuwa huru kufanya mambo yao wenyewe, wengine waliitafsiri hali hii kama penzi kubwa sana, yuko aliyeniambia “mpenzi wangu ananipenda sana, yani hawezi niacha mwenyewe, kila sehemu anataka niende nae” baada ya muda mtu huyu aligundua kuwa ile ilikuwa ni ujanja wa kuficha uhalisi wake na kuzuia mazingira ya mpenzi wake wa kike kugundua au kupewa taarifa za tabia zake, na kwa muda mrefu hakugundua mpaka siku alipo pata tarifa za ukweli na ukawa mwisho wa mahusiano yao, tena mwisho wenye uchungu sana. Kuwa macho sana na tabia za mpenzi wako kukuchunguza sana unapotoka, ulipokuwa, ulikuwa nanani, mlifanya nini, nani mwingine alikuwepo, unaenda wapi, kwa muda gani. Yawezekana yote hii ni hali ya kujilinda au kujihisi mdhambi (guilty conscious) inayomsumbua.
7. Mabadiliko katika tendo la ndoa:
Jambo hili laweza kujidhihirisha katika picha mbili tofauti. Kwa kawaida wapenzi huwa na mazoea fulani katika tendo la ndoa, kwa muda waliokaa pamoja kila mmoja humfahamu mwenzake kwa kiasi fulani. Inawezekana likawa jambo la kushangaza pale ambapo gafla unamuona mpenzi wako anapoteza kabisa hamu ya tendo la ndoa, au hata mnapokuwa katika tendo hilo humuoni akifurahia bali anakuwa kama anayelazimishwa au kutohamasishwa na chochote. Kwa upande mwingine unaweza ukakuta mpenzi wako anakuja na ujuzi wa gafla katika mahusiano yenu ya tendo landoa, hali yake ya kukutamani inazidi gafla, anahitaji mapenzi mara kwa mara na hata mnapokuwa katika tendo hilo anadhihirisha utaalamu wa tofauti na ule uliouzoea. Hali hizi mbili zifanyike tahadhari katika kukusaidia kuyatazama mahusiano yenu.
8. Marafiki wa mpenzi wako kukukwepa:
Ni hali yakawaida kuwa karibu au kuzoeana na marafiki wa mpenzi wako, maranyingine mtawasiliana nao kutaka kujua aliko mpenzi wako au kinachoendelea kwao. Inabidi ujiulize sana pale inapotokea gafla wale marafiki wa mpenzi wako uliowazoea, uliokuwa unawapigia simu wakati wowote leo wana kukwepa, na hata simu hawapokei na maranyingine wakipokea hawakupi taarifa yakueleweka au wanakudanganya. Hii yote inawezekana wanamlinda rafikiyao, au wanakosa cha kujibu maana wanajua uhalisia wa kinachoendelea.
9. Kuzungumza sentensi za kutatanisha:
Kama nilivyosema awali, wapenzi wengi hujuana kwa mengi, ikiwemo pia namna ya kuzungumza au kuonyesha hisia. Unaweza kukuta katika mapenzi yenu mpenzi wako anaanza kuwa na sentensi ngumu na zisizo kuwa na msingi kwa mfano anasema “kwa jinsi hii sidhani kama tutafika” “mi siamini kama mapenzi yanadumu” “yani ndio maana watu wanashindwa kukaa na mpenzi mmoja” na maranyingine anaweza kukuuliza baadhi ya maswali moja kwa moja ili kukuona utajibuje. Sentensi hizi zina chanzo moyoni, kuwa macho.
10. Kuzidi kwa tabia za kutoonekana au kuponyoka:
Yawezekana mpenzi wako alikuwa na tabia ya kuwepo nyumbani mida isiyokuwa ya kazini au wikiendi, muda mwingi alipenda kuwa na wewe na akiaga basi atasema anakwenda wapi na akimaliza hurudi mapema kwa sababu anakiu ya kuwa nawewe, mara gafla sikuhizi haagi anakwenda wapi, ukiuliza inawezakuwa vita. Anakuwa na vijisafari vingi na vijisababu visivyoisha vya kumuwezesha kuponyoka. Sehemu ya kwenda na kurudi lisaa limoja anaweza kuchukua nusu siku, kila ukiuliza atakwambia nakuja, niko njiani, kuna foleni, nimekwama, na sababu nyingine nyingi sana. Ukiona haya yanazidi ujue kuna la zaidi ya foleni, na hizo sababu zote zinazotolewa zinafunika jambo.
11.Tabia za kuficha fedha:
Ninafahamu fika kwamba suala la uwazi katika mambo yanayohusiana na fedha na matumizi ni tatizo kubwa kwa wapenzi wengi, wengi wamegombana na hata kuachana kuhusiana na jambo hili. Japokuwa hili ni tatizo kwa wengi lakini wako wapenzi ambao wamekuwa na tabia ya kuambiana kwa uwazi matumizi na mapato yao, hakuna kitu wamefanya kuhusu fedha zao pasipo kuambiana na hivi ndivyo mlivyozoeshana, mara ghafla mmoja anaanza kuwa na siri kuhusu fedha zake au matumizi yake, na wala hapendi kuulizwa ulizwa kuhusu suala hilo. Tabia hii ikidhihirika katika mapenzi yenu usichelewe kuchunguza maana kwa kukaa kimya unaweza kujikuta umechelea mwana na maji ya moto.

No comments