Mnyika Aongea na Waandishi Ngome kuu ya UKAWA, Awajibu NEC Kuhusu Mazingira ya Wizi wa Kura 25 Oct
Mnyika: Jaji Lubuva Jana amejibu kwa wepesi tuhuma za wizi wa kura
Mnyika: Lubuva anasema ukishapiga kura rudi Nyumbani. Nawaomba vijana na wapiga kura wengine waipuuze kauli ya Jaji Lubuva!
Mnyika: Jaji Lubuva amedai yupo tayari kuziba mianya ya wizi wa kura.Nitataja mianya hiyo ili Jaji Lubuva ajibu masuala haya!
Mnyika: Matokeo ya Rais kubandikwa kituoni sio jambo jipya. Ni suala la kisheria. Nawaomba watu wasome sheria ya Uchaguzi
Mnyika: Masanduku ya kura kupelekwa kituo cha majumuisho sio jambo Jipya.
Mnyika:Lubuva anasema matokeo yatascaniwa jimboni.Hili sio jambo jipya. Mwaka 2010 matokeo yaliyoscaniwa yalikuwa tofauti na karatasi halisi
Mnyika: Jaji Lubuva aseme hadharani, ni lini wataalamu wetu wa IT wakakague na kuhakiki mfumo wa kutuma matokeo ili kuepuka goli la mkono
Mnyika: mfumo wa kujumlisha kura mwaka 2010 ulikuwa na mapungufu makubwa yaliyopelekea uchakachuaji wa kura!
Mnyika: Jaji Lubuva amesema uhakiki umefungwa, kuna jambo kubwa limejificha.Kama hakuna uhakiki daftari limeshakuwa la kudumu!
Mnyika: Mpaka tunavyozungumza hatujakabidhiwa daftari la kudumu la wapiga kura, Takwimu zinazotolewa idadi ya wapiga kura haziaminiki!
Mnyika: Tume iseme ni kwa nini mpaka sasa hawajatoa nakala za "soft copies" kwa vyama vya siasa ili wazihakiki?Hapa bao la mkono limejificha
Mnyika: UKAWA na vyama vingine Lazima viende kuhakiki Database ya Tume Makao makuu. Kwanini Lubuva hataki sisi tuende kuhakiki?
Mnyika: Jaji Lubuva anasema ipo kamati ya IT, muulizeni hiyo kamati ya IT ya vyama vya siasa inaundwa na nani?
Mnyika: Majeshi kuandikisha namba za askari, IGP alikiri jeshi kufanya hivyo kwa baadhi ya mikoa, kuna kitu kimejificha!
Mnyika:IGP alikiri suala hili limefanyika, msemaji wa TPDF alikanusha, kauli zao zilikinzana.Tume iseme ni kwanini majeshi yaliandika namba?
Mnyika: Suala la kuhamisha watumishi wa Tume, limeamia kwa wakurugenzi baada ya Rais, kuteua mkurugenzi Mpya!
Maswali: David Radio5: Wapiga kura wa Mara ya kwanza, na wasiojua utaratibu je wanabakia wapi baada ya kupiga kura?
Mnyika: Wapiga kura, wawe makini kuhakikisha wanapiga kura Siku ya tarehe 25 Oktoba!
Mnyika: Daftari la kudumu halitolewi kwa wakati ili kuruhusu goli la mkono!
Mnyika: wapiga kura wajielekeze kuangalia majina ndani ya daftari la wapiga kura na sio orodha ya wapiga kura inayobandikwa nje ya kituo!
Mnyika: Orodha ya wapiga kura inayobandikwa nje ya kituo inaandaliwa na manispaa, na daftari analopewa wakala limeandaliwa na Tume
Mnyika: Tume itoe Daftari la kudumu la wapiga kura, Jaji Lubuva amesema atalitoa daftari Siku 4 kabla ya Uchaguzi, hapa amejichanganya!
Mnyika:Hatua ya pili ni kutoa 'permanent voter register' hili ilipaswa kutolewa mapema
Mnyika: Kuna madaftari mawili, provisional voter register, hili tulitakiwa kupewa kabla ya uhakiki wa wapiga kura, hili hatujapewa!
Mnyika: Rai yangu kwa wana UKAWA, wasikate tamaa kufuatia matamko ya mawaziri mbalimbali
Mnyika:Juu ya matumizi ya vyombo vya Serikali kujihusishanaUchaguzi, linaongozwa naraisi,Bunge limevunjwa ila baraza la mawaziri linaendelea
Mnyika: Iundwe kamati ya pamoja ya vyama vya siasa ya IT ikakague Daftari na kuliboresha ili kuzuia goli la mkono!
Mnyika: Swali la1: Tulianza kusema haya mambo mapema, waliamua kufumba masikio na macho!
Maswali:Fred kutoka Mtanzania: Kisheria mnatakiwa mpate soft copy ya Daftari baada ya Muda gani?
Maswali: Francis kutoka ATN: suala la uhakiki wa BVR hamuoni Siku zimebaki chache na kwanini msingeliibua suala hili mapema?
Mnyika: Tume iliwahi kukiri kuwa haiko huru mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, WaTZ wasikubali faster faster hii.
Mnyika: Wanapeleka huu mchakato faster faster, rai yangu tusisubiri tarehe 25 Oktoba, tuanze sasa kudhibiti goli la mkono!
Mnyika: Ndani ya nchi tunao watazamaji wasisubiri mpaka Uchaguzi uishe, waende Tume kutazama mfumo huu wa ujumlishaji wa kura
Mnyika: Nawaomba 'Waangalizi wa Uchaguzi' watoe ripoti zao mapema juu ya haya masuala!
Mnyika: Tume ya Uchaguzi sio Mali ya watu binafsi, ni tume ya Taifa letu.
Mnyika: Kijana ukishaona matokeo yamebandikwa, piga picha matokeo hayo na uyatume kwenye WhatsApp!
Mnyika: Kama kuna MTU ataniita mchochezi kwa kusema 'first time voters' wakae mita 200 kusubiria matokeo basi atangulie mahakamani,
Mnyika: First time voters, kukaa ndani ni kosa kisheria, kukaa nje si kosa kisheria, kisheria wanakaa mita 200!
Maswali: David Radio5: UKAWA mtafanya nini endapo tume haitafanya mnayosisitiza wafanye?
Mnyika: Nasisitiza BVR ni Bomu la kufungwa bao la mkono, yote tuliyosema yazingatiwe na wahusika!
Maswali: Prosper - The Guardian: Mnataka wataalamu wa IT wakakague daftari pekee, vipi kuhusu ukaguzi wa idadi ya kura zilizopigwa?
Mnyika: Kama Tume haitasikiliza haya tunayosema wanajitengenezea mazingira ya kupelekwa ICC!
Mnyika: Local monitors wa Uchaguzi wapo wachache, wanasubiria matokeo majimboni, kila mpiga kura lazim awe monitor!
Mnyika: Nje ya kituo cha kupiga kura sisi wapenda Amani, tutawalinda mawakala wetu, wasirubiniwe kupokea hongo ndani ya vituo vya Uchaguzi!
Mnyika: Marando alisema atatangaza matokeo, sasa kwa sababu anaumwa yupo hospitali Mimi Mnyika nitayatangaza.
No comments