Header Ads

Mchakamchaka wa kampeni, Dr. Magufuli leo azua mafuriko Uwanja a jamuhuri-Morogoro, Mzee Makamba amchana Lowassa live

Dr Magufuli ameongeza kuwa yeye si mwanasiasa mzuri bali ni mtendaji zaidi na kwamba baraza la mawaziri atakaloliunda litakuwa ni baraza la mawaziri la kuwatumikia wananchi kwa kutatua kero zao hasa wale wa hali ya chini na kuwataka watakaoteuliwa katika baraza lake wajipange.
Katika mkutano huo ambao umehudhuriwa pia na mwenyekiti wa chama hicho taifa Mh Dr Jakaya Kikwete amewahakikishia watanzania kuwa hawatajuta kumchagua Dr Magufuli kuwa rais wa awamu ya tano kwa kuwa ni mwadilifu na mzalendo na kwa kuchaguliwa kwa Dr Magufuli yeye rais Kikwete atapata usingizi mwema.
Dr Magufuli amefanya pia mikutano katika maeneo ya Ruaha, Mikumi, Kilosa na kisha Morogoro mjini ambapo baadhi ya waliokuwa viongozi waandamizi wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema akiwemo mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Kilosa Bwana Selemani Simba, katibu wa Chadema wilaya ya Kilosa Ibrahimu Selemani na katibu wa jimbo kilosa kati Bwana Musa Ngongi.
Mchakamchaka wa kampeni za uraisi zikizidi kupamba moto, leo hii Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia CCM Ndugu John Makufuli ametia tim Manispaa ya Morogoro.
Akiwahutubia maelfu waliofurika katika uwanja wa Jamhuri, Ndugu Magufuli ameahidi kushughulikia tatizo la ajira kwa kuhakikisha anafufua viwanda vilivyokufa ili kuhakikisha wakazi wa Morogoro wanapata ajira.
Aidha Mh: Magufuli maarufu tingatinga, amesema katika uongozi wake atahakikisha anawashughilikia wala rushwa hasa mapapa ya rushwa ili kuhakikisha anaiweka Tanzania yenye usawa.
Mgombea Ubunge Morogoro Mjini ndugu Azizi Abood
Mzee Yusuph Makamba
Mgombea urais kupitia CCM Dr John Pombe Magufuli amesema serikali yake itatilia mkazo suala la ukusanyaji wa kodi hasa kwa wawekezaji wa nje pamoja na kuangalia upya misamaha ya kodi ili kuiwezesha serikali kukusanya fedha nyingi zitakazosaidia kutoa huduma za kijamii kwa ajili ya maendeleo ya watanzania.
Dr John Pombe Magufuli ameyasema hayo katika uwanja wa amhuri uliopo mkoani Morogoro wakati akinadi sera zake kwa mamia kwa makumi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo ambapo amempongeza rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuongeza mapato ya serikali na kuongeza kuwa serikali yake itaongeza mapato ya serikali kwa kuangalia upya suala misamaha ya kodi kwa wawekezaji hususani wa kigeni.

Sehemu ya wakazi wa Morogoro


Mwenyekiti wa Wilaya ya Morogoro Innocennt Karogeres
Maelfu ya wakazi wakimsikiliza Magufuli 
 Nukuu: Mzee Makamba "Lowassa alitaka kuondoka CCM tangu 1995, Nikamsihi, alishakataliwa kutokana na ufisadi wake. Namuomba kwenye mdahalo, tuliushangaa utajiri wake akiwa mdogo, Hatufai"
Kikwete- " Magufuli anatosha"

No comments

Powered by Blogger.