Header Ads

Andre Ayew ndiye mchezaji bora wa EPL mwezi huu

Bila ubishi kila mtu ameona jinsi Andre Ayew alichokifanya na club yake ya Swansea katika mwezi huu wa nane ambao ndio wa kwanza kwenye ligi ya 2015/16. Jamaa huyu amesajiliwa na Swansea na ameshatupia magoli mawili kwa ajili ya timu yake na kusaidia sana kwenye ushindi wa kila mechi timu yake inayocheza pamoja na mechi dhidi ya Manchester united.Ayew amechukua award hiyo akimpita mchezaji mwenzake Bafetimbi Gomis na mchezaji wa Manchester city David Silva pamoja na Aleksandar Kolarov.
 
“Najiskia vizuri kushinda hii tuzo na inatokana na kazi kubwa tuliyofana pamoja kwenye kikosi chetu. Hii ni zawadi ya timu nzima kwasababu tumefanya sana kazi kubwa kujiandaa tangu pre season hadi sasa”, alisema Andre Ayew

No comments

Powered by Blogger.